HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 16, 2017

Halotel Yawezeshwa Wafanyabiashara Kutangaza Bidhaa zao Bure kwa Simu

Meneja Uendelezaji Biashara Kitengo cha Huduma za Ziada wa Halotel, James Kulwijira akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye uzinduzi wa huduma itakayo wawezesha wateja wa Halotel ambao ni wafanyabiashara kutangaza biashara zao bure kwa kutumia huduma mpya inayojulikana kama Halo SAINI. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Halotel, Stella Pius akishuhudia. Meneja Uendelezaji Biashara Kitengo cha Huduma za Ziada wa Halotel, James Kulwijira akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) katika uzinduzi wa huduma itakayo wawezesha wateja wa Halotel ambao ni wafanyabiashara kutangaza biashara zao bure kwa kutumia huduma mpya inayojulikana kama Halo SAINI. Kushoto ni Caroline Majaliwa, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Ziada wa Halotel na Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Halotel, Stella Pius (kulia). Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Halotel, Stella Pius akionesha kwa wanahabari (hawapo pichani) baadhi ya zawadi ambazo wateja wa Halotel watakuwa wakijishindia kila watakapokuwa wanaweka muda wa maongezi na kubahatisha zawadi.

 KUELEKEA kukua kwa teknolojia ya mawasiliano nchini kumeendelea kuwawezesha watanzania kupata nafasi ya kunufaika na huduma mbalimbali zinazotolewa na mitandao ya simu, Mtandao wa simu wa Halotel umezindua huduma itakayo wawezesha wateja wake ambao ni wafanya biashara kuweza kutangaza biashara zao bure kwa kutumia huduma mpya iliyozinduliwa na kampuni hiyo inayojulikana kama Halo SAINI. 

huduma hii inamuwezesha mteja wa mtandao huo, ambae tayari amejiunga na huduma hiyo kutengeneza ujumbe maalum kuhusu biashara yake na kila atakapo piga simu au kupigiwa, mhusika atapata ujumbe maalum utakaomueleza kuhusu biashara husika ya Mteja wa Halotel. 

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Huduma hiyo, Mkuu wa Kitengo cha huduma za Ziada wa Halotel, Caroline Majaliwa amesema kuwa mapinduzi hayo ya kiteknolojia yatawawezesha mamilioni ya wafanya biashara wanao tumia mtandao huo kuweza kutangaza biashara zao kwa wale wanao wapigia na hata wanaopokea simu zao.

 “Licha ya kuendelea kuwa na huduma nzuri za kuvutia, tumeendelea kubuni na kuja na huduma zitakazo wawezesha wateja wetu kuendelea kufurahia huduma zetu kadha wa kadha na sasa kuwawezesha kutangaza biashara zao kwa watu wanao wapigia au kupokea simu zao, ambapo baada ya kuwezesha huduma hiyo wataweza kupokea ujumbe maalum ambao atahitaji yeye mwenyewe ufike kwa wateja wake”. Alisema Majaliwa. Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Halotel, Stella Pius akielezea namna ambavyo wateja wa Halotel watakuwa wakijishindia kila watakapokuwa wanaweka muda wa maongezi na kubahatisha zawadi kwa wanahabari (hawapo pichani).

Aidha Majaliwa aliongeza kuwa, ili mteja aweze kufurahia huduma hiyo atatakiwa kutuma neno ON kwenda namba 15614 kujiunga, na kisha atapaswa kutuma neno SAINI kisha ujumbe ambao anataka watu waupate pindi watu watakapokuwa wakimpigia au yeye kuwapigia kwenda kwenye namba 15614. 

Kwa Upande wake, Meneja Uhusiano wa Kampuni hiyo, Stella Pius amesema licha ya kuwawezesha wateja wao kuweza kutumia nafasi hiyo kutangaza biashara zao, Amesema kuwa wameamua kuwazawadia wateja wao wote ambao wameendelea kuwaunga mkono, kwa kuwawezesha kushinda zawadi mbalimbali kila watakapokuwa wanaweka muda wa maongezi. 

“Tunathamini sana mchango wa wateja wetu na tumeamua nasi kuendelea kuwazawadia kwa kuwawezesha kujishindia zawadi kem kem kila wanapoweka vocha za mtandao wa Halotel. 

Kila Mteja wa Halotel atakapoweka vocha katika simu yake atapokea ujumbe wenye namba ya bahati ambayo atatakiwa kuituma kwenda namba 0901220004 na ataingia katika droo ambayo itamuwezesha kujishindia zawadi ya muda wa Maongezi au Smartphone zitakazo kuwa zinatolewa kwa siku, wiki na kila mwezi kwa washindi watano (5),” Alisema Pius na kuongeza; “Tutakuwa tunachezesha droo kwa siku, wiki na kila mwezi na washindi watajishindia muda wa maongezi wa hadi shilingi elfu 50,000/= pamoja na simu za Smartphone zenye teknolojia ya hali ya juu,” Hili linatuwezesha sisi kuendelea kuthamini mchango wa wateja wetu ambao wameendelea kutuunga mkono siku hadi siku, Alihitimisha Pius. 

Pamoja na huduma hizo, kampuni hiyo pia imeboresha huduma nyingine ambazo zitawawezesha wateja wa mtandao huo, kuweza kusikiliza redio katika maeneo mbalimbali yaliyo na mtandao wa Halotel, hata kama hakuna masafa ya FM/AM ya radio hiyo, katika eneo husika. 

Huduma nyingine iliyozinduliwa sambamba na huduma hizo ni pamoja na huduma ya Halosoka ambayo itamuwezesha mteja wa mtandao huo kuweza kupata matokeo ya mpira wa miguu papo hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad