HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 5, 2017

Ajali ya mabasi, lori yajeruhi 12 Mlima Kitonga

Watu 12 wamejeruhiwa na watatu kati yao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa baada ya kutokea ajali iliyohusisha magari mawili ya abiria na lori moja, katika eneo la Mlima wa Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani hapa.
Akizungumza na gazeti hili baada ya kutokea kwa ajali hiyo Saa 7 mchana leo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi amesema magari yote matatu yaliyohusika kwenye ajali hiyo yalikuwa yakienda jijini Dar es Salaam.
Ameyataja mabasi yaliyohusika kwenye ajali hiyo kuwa ni ya Kampuni ya Happy Nations, Abood na gari moja la mzigo.
Mjengi amesema katika ajali hiyo watu 12 walipata majeraha na watatu kati yao wamefikishwa Hospitali ya Rufaa ya mkoani Iringa kwa matibabu na tisa kati yao walitibiwa na kuruhusiwa kutoka hospitali.
Kamanda huyo ametaja chanzo cha ajali kuwa ni dereva wa gari la Abood lililokuwa nyuma ambaye aliligonga basi la Happynations ambalo nalo gari lilikuwa mbele yake na kusababisha magari yote kuserereka na kutoka pembeni mwa barabara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad