HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 6 March 2017

AHMADA SIMBA KUITWA KAMATI YA MASAA 72

Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Alfred Lucas.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

MWAMUZI wa mchezo baina ya Yanga na Ruvu Shooting Ahmada Simba anatarajiwa kuitwa kwenye kamati ya masaa 72 pindi pale atakapowasilisha barua yake ya utetezi kuhusiana kukataa goli na kumpatia kadi ya njano Obrey Chirwa.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Yanga kutoka nchini Zambia alipatiwa kadi hiyo katika dakika ya 43 baada ya kufunga goli na mwamuzi kulikataa goli hilo ambalo baadae lilikuja kuonekana halina matatizo.

Katika mchezo huo wa ligi kuu Vodacom, mwamuzi Ahmada Simba alimpatia kadi ya pili Chirwa na kupelekea kupata nyekundu lakini Yanga waliweza kutoka na ushindi wa goli 2-0 dhidi  ya Ruvu Shooting.

Akizungumza na Globu hii, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) Alfred Lucas amesema kuwa kamati hiyo itakaa pindi watakapopokea utetezi wa mwamuzi huyo na kisha kutoa maamuzi ya juu yake.

Lucas amesema, kabla ya kamati ya masaa 72 kukaa kwa ajili ya kujadili mechi za Simba dhidi ya Yanga, Ruvu dhidi ya Yanga tayari uongozi wa Yanga ulishatuma barua juu ya malalamiko ya kadi ya njano ya kwanza aliyopatiwa Chirwa na kutaka kuangaliwa tena.

Baada ya kadi ya kwanza ya njano kufutwa moja kwa moja inapelekea kufutika kwa kadi nyekundu ya mshambuliaji huyo kutoka nchini Zambia.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad