MKUU
wa mkoa wa Iringa mwalimu Amina Masenza amewaonya watumishi wa
serikali ambao wanakwepa kushiriki mazoezi ya pamoja katika uwanja
wa Samora na kuwa kuanzia sasa mtumishi atakayekwepa kushiriki
kubanwa .
Alisema
pamoja na kuwa mazoezi hayo ni kwa ajili ya afya za kila mmoja
kujikinga na maradhi yanayosababishwa na kutofanya mazoezi ila bado
mazoezi hiyo ni utekelezaji wa agizo la makamu wa Rais kwa kila
mtanzania .
Hivyo
alisema kutokana na baadhi ya watumishi hasa wanawake kukwepa
mazoezi hayo anaandaa mkakati wa kuwabana watumishi wote wanaokwepa
mazoezi kwa kuitisha mazoezi siku ya kazi ili wale ambao
watashindwa kufika watawajibishwa .
"Naangalia
ni siku gani ambayo itakuwa ni siku ya kazi kama ijumaa ama siku
nyingine yeyote ambayo nitaitisha mazoezi kuanzia ofisi yangu hadi
Samora kwa kila mtumishi kushiriki na siku hiyo hata ofisini
watumishi wakichelewa ni sawa lengo kuweza kufanya mazoezi na
kutekeleza agizo la serikali ......nashangazwa sana awali wanawake
ndio ambao walikuwa wakifika kwa wingi mazoezini ila leo hii idadi
ya wanawake imepungua ukilinganisha na wanaume ....nawashangaa sana
wanawake wanaokwepa mazoezi wakati ndio ambao wanakula vitu vyenye
mafuta "
Hivyo
alisema kuanza sasa kila mtumishi wa serikali lazima kufika katika
mazoezi na utawekwa utaratibu wa kuorodhesha majina kila idara ya
watu wanaoshiriki mazoezi .
 |
Mkuu wa mkoa wa Iringa mwalimu Amina Masenza (wa tatu kushoto) akiongoza mazoezi ya viungo katika uwanja wa samora Leo wa pili kushoto ni katibu tawala wa mkoa wa Iringa wamoja Ayubu |
 |
DC Iringa Richard Kasesela wa kwanza kulia akishiriki mazoezi ya riadha kutoka uwanja wa Samora |
 |
Washiriki wa mazoezi wakiwasili ufisi ya RC Iringa wakitokea uwanja wa Samora |
 |
Afisa michezo mkoa wa Iringa Kenedy Komba akiorodhesha majina ya wakuu wa Idara walioshiriki mazoezi leo ni kuwabana wamnaokwepa mazoezi |
 |
Wanamazoezi wakitoka uwanja wa samora |
 |
Mkazi wa Iringa akiwa amebeba pombe aina ya komoni asubuhi ya leo pombe hii inatengenezwa kwa mahindi jambo ambalo serikali ya mkoa imepigamarufuku matumizi mabaya ya chakula |
 |
Mkazi wa Iringa akipishana na washiriki wa mazoezi huku akiwa amebeba pombe ya komoni inayotengenezwa kwa mahindi |
 |
RAS Iringa na RC Masenza kulia wakiwa katika mazoezi |
 |
RC Iringa Amina Masenza kulia akiongoza mazoezi saa 12 asubuhi ya leo |
 |
Afisa habari Manispaa ya Iringa Sima Bingilengi kushoto akiwajibika |
 |
Mwanahabari Manispaa ya Iringa Janeth Matondo kulia pia akishiriki mazoezi |
 |
DC Kasesela katikati wa pili kulia akiwa na wadau wa kwanza kulia ni Geofrey Mungai |
 |
Mzee Vitus Mushi akiwajibika mazoezini
|
 |
DC Iringa Richard Kasesela wa tatu katikati kulia akiwa na mkurugenzi Manispaa ya Iringa Dr Wiliam na mwanasheria wa Iringa wa pili kulia |
 |
Na MatukiodaimaBlog |
No comments:
Post a Comment