HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 15 February 2017

Watumishi Muhimbili wamuaga Mama Eda Kapange

Kushoto ni Mama Eda Kapange akikata keki katika hafla hiyo ya kumuaga, keki iliyoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga. 
Watumishi wa afya wamekumbushwa kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia maadili ya taaluma ya kazi ili kuendelea kutoa huduma bora .

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Agnes Mtawa alipokua akizungumza katika hafla fupi ya kumuaga Muhudumu wa afya Mama Eda Kapange aliyekua akihudumu katika Idara ya watoto Hospitalini hapo.

Amesisitiza kuwa suala la kuzingatia maadili ya taaluma hiyo ni muhimu kwani mgonjwa anahitaji upendo na kupewa maneno yenye matumaini na kwamba hiyo pekee ni tiba .

Pia Mkurugenzi Mtawa amemuelezea Mama Eda Kapange kuwa ni mtumishi hodari na mchapakazi hivyo amewataka watumishi wengine kuiga mfano wake kwa vitendo.
Baadhi ya wauguzi na Madaktari wa Idara ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla hiyo.
Baadhi ya viongozi wakimtakia heri na afya njema mama Eda Kapange katika maisha yake baada ya kulitumikia taifa.
Mkurugenzi wa Huduma za Uuguzi na Ukunga Agnes Mtawa akitoa neno katika hafla fupi ya kumuaga Muhudumu wa afya Mama Eda Kapange iliyofanyika katika Hosppitali ya Taifa Muhimbili.
Baadhi ya Wauguzi na Madaktari wa Idara ya watoto wakishangilia huku wakiinua maua juu kama ishara ya upendo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad