HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 28 February 2017

WASANII WATAKIWA KUACHA KUTUMIA MADAWA AMA VILEO KABLA YA KUFANYA KAZI ZAO

 Mwandishi wa habari Mwandamizi kutoka Michuzi Blog , Humphrey Shao akiongea na wasanii na Waandishi wa habari katika jukwaa la sanaa lililoandaliwa na BASATA juu ya tatizo la Dawa za kulevya kwa wasanii wa kwanza kulia ni Snura Mushi na watatu kutoka kushoto  ni Msanii wa Mizengwe Hemed maliyaga(Mkwere Original) na katibu mkuu wa basata , Godfrey Mwingereza .
 Katibu mkuu wa BASATA, Godfrey Mwingereza akizungumza  na wasanii na waandishi habari juu ya kujikwamua katika tatizo la dawa za kulevya
 wadau wa wasanaa na waandishi wa habari wakifatilia
Katibu mkuu wa Baraza la Sanaa Basata akizungumza na wasanii wa filamiu na muziki kabla ya kuingiakatika mkutano.
Na Ripota wa globu ya jamii
Wito umetolewa kwa wasanii kuacha kutumia dawa za kulevya na vileo kabla ya kuanza kufanya kazi zao hili waweze kuongeza weledi wa sanaa kwa hadhira.

Wito huo umetolewa na mwandishi mwandamizi wa Michuzi blog Humphrey Shao, alipokuwa akizungumza na wasanii pamoja na waandishi wa habari katika jukwaa la Sanaa lililoandaliwa na Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA)
Akizungumza katika jukwaa hilo Shao amesema kuwa ameweza kuandika makala nyingi sana zinazousu matatizo ya dawa za kulevya kwa wasani tangu mwaka 2014 lakini mwaka huu 2017 ndipo mambo yote yamekuwa hadharani.
   
 “tatizo la dawa za kulevya kwa wasanii alijaanza leo na wengi wao uanzia na kilevi cha bangi na kupelekea kujingiza kwenye dawa za kulevya hali inayo hatarisha maisha yao na kazi zao za sanaa”amesema Shao.

Kwa upande wake msanii wa muziki wa Bongo Fleva Snura Mushi amesema kuwa amekuwa akishuhudia wasanii wengi ambao awawezi kupanda jukwaani mpaka walewe hali inayopelekea wengi wao kuharibu kazi na kupoteza mashabiki.
Ametaja kuwa mtu ukitumia madawa yakulevya au pombe katika kazi yako inakufanya upoteze umakini ambao unaweza kukupoteza katika ramani ya sanaa na heshima yako kushuka.

Nae katibu mkuu wa BASATA, Godfrey Mwingereza ametoa onyo kwa wasanii wote ambao wanatumia dawa za kulevya na wale upendelea kunywa pombe kupita kiasi na kupanda katika majukwaa ya muziki.

Mwingereza amesema kuwa kitendo cha msanii kupanda jukwaani akiwa amelewa ni kudhalilisha kazi ya sanaa ambayo ni kazi kama ilivyo kazi nyingine na kutaja kuwa ni mara chache sana kuona wakandarasi au madaktari kuona wakiwa katika kazi zao wamelewa kama wasanii wetu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad