HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 3 February 2017

WALIOKAIDI WITO WA RC MAKONDA KUKAMATWA

  Mmoja wa wasanii mahiri wa bongofleva,maarufu kwa jina la kisani T.I.D akiwasili kituo cha polisi kati,wakiitikio wito wa RC Paul Makonda kufika kituoni hapo kwa tuhuma za madawa ya kulevya.

NA Anthony John Glob jamii

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amelitaka jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam kuwakamata wale wote ambao hawajafika kuripoti kituoni hapo kwa kufuatia tuhuma za uuzaji na uvutaji wa madawa ya kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari kituoni hapo makonda amesema kuwa kuna baadhi ya watu ambao walitakiwa kuripoti katika kituo cha polisi kati na hawajafika ambao ni Rashidi makwilo (chidi benzi, Samir Kheri (mr blue) pamoja na wamiliki wa klabu za kuuza pombe.

"kuna watu walio waita lakini hawajafika mpaka sasa hawajafika naliagiza jeshi la polisi kuwakamata na kuwaweka ndani wote ambao hawajafika mpaka juma tatu", amesema 

Sambamba na hayo Mkuu huyo wa mkoa ameongeza majina matatu ya maaskari polisi na wasanii ambao wanatakiwa wakamatwe kwa tuhuma za kushirikiana na wauza madawa ya kulevya pamoja na Vanesa mdee na mwana dada Tunda kufika katika kituo cha kati.

Makonda ametoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kutokomeza hali ya uuzaji na uvutaji wa madawa ya kulevya hapa nchini.
 Mwanadada maarufu hapa jijini Dar,Wema Sepetu  akiwa na mmoja wa wasaidizi wake wakiwasili kituo cha polisi kati,wakiitikio wito wa RC Paul Makonda kufika kituoni hapo kwa tuhuma za madawa ya kulevya
 Mmoja wa wasanii anaetambulika kwa jina la kisanii Babuu wa Kitaa akiwasili kituo cha polisi kati,wakiitikio wito wa RC Paul Makonda kufika kituoni hapo kwa tuhuma za madawa ya kulevya
 Baadhi ya watu waliofika kituo cha polisi kati kujionea watuhumiwa mbalimbali wa Madawa ya kulevya walioitikia wito wa kuitwa kutoka kwa RC Paul Makonda
  Mmoja wa wasanii mahiri wa bongofleva,maarufu kwa jina la kisani T.I.D akiwasili kituo cha polisi kati,wakiitikio wito wa RC Paul Makonda kufika kituoni hapo kwa tuhuma za madawa ya kulevya.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad