HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 9 February 2017

WAFANYABIASHARA WAKUTANA DAR KUJADILI NAMNA YA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA NCHINI

Mkutano wa wafanyabiashara uliofanyika jijini Dar es salaam umefanyika leo kwa mafanikio makubwa.Akizungumza wakati wa mkutano huo ulioandaliwa na Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo na EAG Group mgeni rasmi Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dr. Adelhelm Meru alipongeza mkutano huo kwa kuwaleta pamoja wadau wa biashara kujadili masuala yenye msingi. Pia alisisitiza azma ya Serikali ya awamu ya tano katika kuboresha mazingira ya biashara Nchini.
Kwa upande wake Rais wa Chemba Ndibalema Mayanja alieleza umuhimu wa wafanya biashara kuwa na sauti moja na kukuza biashara.Mkutano huo ulishirikisha Viongozi wa makampuni, Mabalozi na Taasisi mbalimbali za serikali.
Mada mbalimbali ziliwasilishwa ikiwemo mazingira ya biashara, kufanya biashara na China, Safari ya Biashara Italy na Turkey, Huduma za Banki ya NMB na uwekezaji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad