HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 18, 2017

UKARABATI WA MELI YA MV CLARIAS WAKAMILIKA, KUANZA KUTOA HUDUMA MWISHONI MWA MWEZI HUU

Meli ya MV. Clarias inayomilikiwa na Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), inayofanyiwa ukarabati katika bandari ya Mwanza ambao ukarabati wake utakamilika mwanzoni mwa wiki ijayo na kuanza kutoa huduma mwishoni mwa mwezi huu. 

Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya uchukuzi), Eng. Dkt. Leonard Chamuriho ameipongeza kampuni ya huduma za meli nchini (MSCL), kwa kukarabati meli zake kwa kutumia fedha za ndani na hivyo kuhuisha utendaji kazi wa kampuni hiyo.

Akizungumza jijini Mwanza mara baada ya kukagua huduma zinazotolewa na kampuni hiyo Eng. Dkt. Chamuriho amesema Serikali itawekeza kikamilifu kwenye kampuni hiyo baada ya kuridhika na utendaji uliopo sasa.

“Fanyeni kazi kwa bidii na fikra mpya Serikali inashughulikia kwa karibu suala la mishahara yenu na stahili nyingine” amesema Eng. Dkt. Chamuriho.

Hivi karibuni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alimteua Kaimu Meneja Mkuu mpya wa kampuni hiyo Bw. Eric Hamisi ambaye kwa kushirikiana vema na menejimenti na wafanyakazi wamewezesha kuongeza mapato kwa kwa asilimia 100.

Kampuni ya huduma za Meli MSCL ni moja ya kampuni ya Meli yanayomilikiwa na Serikali kwa asilimia 100 na kusimamiwa na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Sekta ya Uchukuzi na inatoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika maziwa makuu yaliyopo nchini Victoria,Nyasa na Tanganyika
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng.Dkt, Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Eric Hamisi (mwenye shati jeupe), wakati alipokagua ukarabati wa Meli ya MV. Clarias.
Fundi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), akiendelea na ukarabati wa meli ya MV Clarias ambayo ukarabati wake utakamilika mwishoni mwa wiki na kuanza kazi ya kutoa huduma katika Ziwa Victoria.
Nahodha wa Meli ya Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Swedi Ruganza akitoa maelezo ya namna nahodha anavyoendesha meli kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng. Dkt. Leonard Chamuriho (katikati), alipofanya ukaguzi wa ukarabati wa meli hiyo jijini Mwanza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Sekta ya Uchukuzi, Eng.Dkt. Leonard Chamuriho, akitoa maelekezo kwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Huduma za Meli (MSCL), Bw. Eric Hamisi (wa pili kutoka kushoto), mara baada ya kuangalia kina cha maji katika bandari ya Mwanza. PICHA NA Biseko Lisso Ibrahim, WUUM (U)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad