HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 7 February 2017

TID, Recho, Tunda waachiwa kwa dhamana, Wema abaki

 Watuhumiwa wa biashara na matumizi ya dawa za kulevya waliotajwa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaamm, Paul Makonda, Jumanne hii, February 7, 2017 wamefikishwa katika mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu tuhuma zinazowakabili.

Mastaa hao wakiwemo TID, Nyandu Tozi, Babu wa Kitaa, Romy Jones, Tunda, na wengine, wameachiwa kwa sharti la dhamana ya shilingi milioni 10 kila mmoja na watakuwa wakiripoti kwa mwezi mara mbili huku wakiwa katika uangalizi wa jeshi la polisi kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Hata hivyo watuhumiwa wengine wakiwemo Petit Man, Said Alteza, Lulu Diva na wengine wametakiwa kuweka dhamana ya shilingi milioni 20 na watakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha miaka mitatu. Iwapo watuhumiwa hao watashindwa kufuata masharti hayo watarudishwa tena mahakamani.

Hali imekuwa tofauti kwa Wema Sepetu ambaye ameendelea kukaa rumande baada ya msako kubaini msokoto wa bangi nyumbani kwake na hivyo kuongezwa kosa jingine zaidi ya lile la awali, ambapo sasa inasubiriwa uchunguzi kukamilika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad