HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 21 February 2017

TAKWIMU YA MAJANGA YA MOTO MKOA WA MBEYA KWA MIAKA SITA ILIYOPITA...  SGT Weston Paul Ngaponda akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari wakati akijibu maswali yaliyoulizwa na Bw. Fadhiri Aticki Mr Pengo kutoka Michuzi Blog na Michuzi Tv.
Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Mbeya limetoa Takwimu ya Ajali za Moto zilizotokea ndani ya miaka 6 kuanzia 2011 mpaka 2016.
Akizungumza na waandishi wa habari Sajenti Weston Paul Ngaponda kwa niaba ya Mkuu wa Operesheni Zimamoto Mkoa wa Mbeya amesema Jeshi la Zimamoto na Uokozi Mkoani Mbeya linafanya majukumu yake kwa weredi mkubwa na kwa mafanikio makubwa.


SGT Ngaponda ametoa Takwimu za Ajali za moto kwa muda wa miaka sita na zipo kama ifuatavyo:-
1.Mwaka 2011,Matukio ya Moto yalikuwa  jumla 54 kwa wastani wa Matukio matano kwa mwezi.
2. Mwaka 2012, kwa mwaka mzima matukio yalikuwa jumla 88, kwa wastani wa matukio 7 kila mwezi.
3. Mwaka 2013, Jumla ya matukio ya moto yalikuwa 50, kwa wastani wa matukio manne kila mwezi.
4. Mwaka 2014, Jumla ya matukio ya moto yalikuwa 52, kwa wastani wa matukio manne kila mwezi.
5. Mwaka 2015, Jumla ya matukio ya moto yalikuwa 74, kwa wastani wa matukio 6 kila mwezi.
6. Mwaka 2016, Jumla ya matukio ya moto yalikuwa 65, wastani wa matukio matano kila mwezi.
SGT Ngaponda akiongea na wanaHabari amesema kwa tathmini zao ni kwamba matukio ya ajali za moto yanazidi kupungua Mkoani Mbeya huku akiwasifu wananchi kwa ushirikiano wanaowaonyesha pindi majanga ya moto yatokeapo. Aidha,SGT Ngaponda amesema Jeshi la Zimamoto limekuwa likitoa elimu kuhusu majanga ya moto pindi litokeapo tatizo sehemu ili kusaidia kupunguza hatari hizi kwa siku za usoni. Pia amesema vyanzo vya moto daima husababishwa na binadamu kwa mitazamo tofauti, inaweza kuwa kwa Ujinga, Uzembe na Uhujumu.
Akitolea maelezo jinsi ya kuepuka majanga ya moto amesema, kwa wale wazembe basi Umakini unahitajika sana pindi watumiapo vitu vinavyoweza kusababisha moto kama mishumaa, taa ya kandiri, matumizi ya umeme na kwa upande wa Ujinga Elimu pekee inaweza kusaidia kuifanya jamii kuwa salama zaidi. SGT Ngaponda amewaomba wananchi wa Mkoa wa Mbeya kujitahidi kutoa taarifa mapema majanga yatokeapo bila kuchelewa kwani wapo wananchi ambao huchelewa kutoa taarifa.
Akihitimisha Taarifa hiyo ametoa wito kwa wananchi hasa waiishio Mbozi kwani wamekuwa na tabia ya udanganyifu kwa kuwapigia simu Jeshi la Zimamoto kuwa kuna janga la Moto kumbe sio kweli na baadhi ya wananchi kuzitumia namba za Zimamoto kwa matumizi yasiyostahiki.
 Wanahabari wakimsikiliza kwa makini SGT Ngaponda wakati akitoa Ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali yahusuyo Jeshi la Zimamoto
MAELEZO NA: THOBIAS OMEGA
PICHA NA: MR PENGO MMG...

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad