HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 21, 2017

SERIKALI YAWATAKA MAAFISA HABARI KUTUMIA NJIA ZA KISASA ZA MAWASILIANO KUTANGAZA MAFANIKO YA SERIKALI

 Mkurugenzi wa Habari na  Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas akizungumza na Maafisa Habari na Tehama wakati wa Mafunzo elekezi ya matumizi ya tovuti kutoka Mikoa 5 na Halmashauri 35 za Mikoa ya Kanda ya Ziwa  yaliyofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekaani (USAID) na kusimamiwa na Ofisi ya      Rais- TAMISEMI,  Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Wakala ya Serikali Mtandao (EGA). Mafunzo hayo yalianza tarehe 9-20 Februari, 2017, kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Rebecca Kwandu. 

Na Ismail Ngayonga 
MAAFISA Habari na Mawasiliano Serikalini katika Mikoa na Halmashauri nchini wametakiwa kutumia njia za haraka na za kisasa katika mawasiliano ikiwemo matumizi ya tovuti na mitandao ya kijamii ili kutangaza shughuli na mafanikio ya sera na mipango ya Serikali kwa wananchi.

Hayo yamesemwa jana Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas wakati wa uzinduzi wa tovuti za halmashauri 35 za mikoa 5 ya kanda ya ziwa inayojumuisha Mikoa ya Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga na Simiyu.

Dkt. Abbas alisema pamoja na kuwepo kwa vyombo mbalimbali vya habari vinavyotumika kufikisha taarifa za habari kwa wananchi ikiwemo magazeti na redio, bado mitandao mitandao ya kijamii ikiwemo barua pepe imendelea kutumia na wananchi wengi zaidi ulimwenguni kwa sasa. 

“Kwa sasa nusu ya watu duniani wapo mtandaoni na hapa nchini kwa mujibu wa ripoti ya TCRA (Mamlaka ya Mawasiliano Nchini) inaonyesha kuwa Watanzania zaidi ya Milioni 19 wapo mtandaoni aidha kwa kutumia barua pepe au kutembelea kurasa za facebook” alisema Dkt. Abbas.

Kwa mujibu wa Dkt. Abbas alisema sifa za Afisa Habari na Mawasiliano wa karne ya sasa ni mwenye uwezo wa kutumia njia za kisasa za mawasiliano, ambazo zitamwezesha kujibu hoja mbalimbali kwa haraka zaidi badala ya kusubiri Serikali kulalamikiwa na wananchi.

Aidha Dkt. Abbas alisema uzinduzi wa tovuti katika mikoa na halmshauri hizo ni kigezo muhimu kitakachotumiwa na Serikali katika kupima wa utendaji kazi wa Maafisa Habari katika kushughulikia kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Akifafanua zaidi Dkt. Abbas alisema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa tovuti za mikoa na halmashauri za Wilaya nchini zinaendelea kuwa hai na zenye taarifa zilizozingatia muda na wakati na hilo litawezekana iwapo Maafisa Habari watatimiza malengo wanayopaswa kujiwekea katika maeneo yao ya kazi.

“Litakuwa si jambo jema tunaona kuwa baada ya miaka 5 tovuti hizi zimesimama, hii haitapendeza sana, hatuna budi tukatambua kuwa Serikali na wafadhili wameweza fedha katika mradi huu, hivyo ni wajibu tukatimize wajibu wetu” alisema Dkt. Abbas.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mji wa Magu, Fundikira Fundikira alisema Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili Maafisa Habari ikiwem ukosefu wa vitendea kazi, ambapo hata hivyo suala hilo lisitumika kama kigezo cha kuwakosesha wananchi taarifa.

Aidha aliongeza kuwa mafunzo hayo yaliyotolewa kwa Watendaji hao wa Serikjali  ni deni kwao hivyo Maafisa Habari na TEHAMA hawana budi kuhakikisha kuwa wanatimiza wajibu wao na kuleta tija iliyokusudiwa katika maeneo yao ya kazi.

“Sisi kama Mkoa tutahakikisha kuwa tovuti hizi tunazisimamia na kuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi wetu, na kuhakikisha kuwa fedha za Serikali na Wafadhili zinaleta tija kwa wananchi wetu”   alisema Fundikira.

Naye Mkurugenzi wa Miundombinu katika Wakala ya Serikali Mtandao (EGA), Benjamin Dotto alisema Maafisa Habari na TEHAMA wanapaswa kuweka taarifa mpya zilizozngatia muda na wakati kwa kuwa suala la upatikanaji ni utekelezaji wa haki ya kimsingi ya binadamu pamoja na utekelezaji wa mikataba mbalimbali ya kimataifa iliyosainiwa Serikali.

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 13-20 Februari, yalifadhaliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID) na kusimamiwa na Ofisi ya Rais- Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wakala ya Serikali Mtandao (EGA).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad