HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 24, 2017

NSSF, PPF zasaini Makubaliano (MOU) na Jeshi la Magereza kwaajili ya Uendelezaji wa Mradi wa Kiwanda cha sukari na shamba la miwa Mbigiri

Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (CGP) Dkt. Juma Malewa (katikati) akizungumza katika hafla ya kusaini Mkataba wa Makubaliano (MOU) kwaajili ya Uendelezaji wa Mradi wa Kiwanda cha sukari na shamba la miwa Mbigiri Mkoani Morogoro, uliosainiwa kati ya Jeshi la Magereza na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF kwa pamoja na Mfuko wa PPF, yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam. kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara akizungumza katika hafla ya kusaini Mkataba wa Makubaliano (MOU) kwaajili ya Uendelezaji wa Mradi wa Kiwanda cha sukari na shamba la miwa Mbigiri Mkoani Morogoro, uliosainiwa kati ya Jeshi la Magereza na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF kwa pamoja na Mfuko wa PPF, yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam.
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini (CGP) Dkt. Juma Malewa akisainiana mkataba wa makubaliano na Mkurugenzi wa Muda wa Kampuni ya Mkulazi Holdings Co. Ltd, Nicander Kileo huku wakishuhudiwa na Wakurugenzi wa NSSF (Prof. Godius Kahyarara) na PPF (William Erio), katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. 
Picha ya pamoja na Watendaji wakuu wa Mifuko hiyo ya NSSF na PPF.
Picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi la Magereza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad