Mfuko wa pensheni wa PPF ulifanya kikao cha Baraza la Wafanyakazi
Mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki. Katika kikao hicho moja ya mada
iliyojadiliwa ni uwekezaji katika kilimo cha miwa na kiwanda cha sukari
katika eneo la Mkulazi mkoani Morogoro ambayo iliwasilishwa na
Mkurugenzi wa Muda wa Kampuni ya Mkulazi Holdings Co. Ltd, Nicander Kileo.
Uwekezaji huo unafanyika chini ya Kampuni ya Mkulazi Holdings Ltd
ambayo ni Kampuni Tanzu ya Mfuko wa Pensheni wa PPF na Shirika la
Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF). Uwekezaji wa kiwanda hiko cha sukari
upo katika eneo lenye ukubwa wa zaidi ya hekari 63,000 na upo katika hatua za awali ambapo unatarajiwa kuzalisha tani 200,000 za
sukari utakapokamilika. Mradi huo utapunguza uhaba wa sukari nchini
na kutoa fursa za ajira kwa Watanzania.
Katika kikao hicho cha Baraza la Wafanyakazi wa PPF Mkurugenzi Mkuu
wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio alimkaribisha
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Prof.
Godius Kahyarara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa
Kampuni ya Mkulazi Holdings Co. Ltd kuelezea mradi wa ubia kati ya PPF
na NSSF.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio ambaye pia ni
Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa PPF (katikati walioketi) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe
wa baraza la wafanyakazi ambapo katika kikao hicho PPF walimkaribisha Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara
kuelezea mradi wa ubia kati ya PPF na NSSF, katika Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa
PPF kilichofanyika mkoani Morogoro mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Prof. Godius Kahyarara
akitoa ufafanuzi juu ya uwekezaji katika viwanda cha Mkulazi ambapo aliwapongeza
wafanyakazi wa PPF kwa kuupokea mradi huo.
Kutoka Kushoto, Mkurugenzi Mkuu Wa Mfuko Wa Pensheni Wa PPF Ndg. William
Erio, Mkurugenzi wa Muda wa Kampuni ya Mkulazi Holdings Co. Ltd. Ndg. Nicander
Kileo ambayo ni Kampuni Tanzu ya Mfuko wa PPF na NSSF na Mkurugenzi Wa Shirika la Taifa Wa Hifadhi Ya Jamii (NSSF) Prof. Godius Kahyarara wakijadiliana
wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa PPF mwishoni mwa wiki.
No comments:
Post a Comment