HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 1 February 2017

MAMELOD SUNDOWN WAAHIDI USHINDI DHIDI YA AZAM

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KOCHA mkuu wa Mamelod Sundown Pitso Mosimane aahidi kuondoka na ushindi katika ardhi ya Tanzania dhidi ya Azam mechi itakayopigwa saa 1 usiku  kwenye dimba la Uwnaja wa Taifa.

Mamelod ambao ni mabingwa wa Klabu Bingwa Barani Afrika wanajiandaa na mchezo wa Super Cup dhidi ya mabingwa wa kombe la Shirikisho TP Mazembe na wakaamua kutafuta mechi za kirafiki ili kujipima nguvu.

Akizungumza walipomaliza mazoezi hayo jana, Mosimane ameweka wazi kuwa timu yake imejiandaa kufanya vizuri kwenye mechi hizi za kirafiki atakazocheza hapa nchini na kikubwa ni kuwa wanajiandaa na mechi dhidi ya Mazembe ambapo inatarajiwa kuw aya ushindani mkubwa sana.

Miaka minne iliyoiputa timu ya Mamelod iliweza kucheza mechi ya kirafiki na Azam nchini Afrika Kusini walipokuwa wameenda kuweka kambi na mshambuliaji wa Azam kwa kipindi hiuko Gaudency Mwaikimba aliweza kuifungia timu yake bao pekee la ushindi dhidi ya Mamelod Sundown.

Baada ya mechi yao dhidi ya Azam , Mamelod watacheza na timu ya African Lyon Februari 3 kwenye Uwanja wa Taifa.
 Kocha mkuu wa Mamelod Sundown Pitso Mosimane akiwa anafuatilia mazoezi ya wachezaji jana katika Uwanja wa Taifa.
Wachezaji wa Mamelod Sundown wakiwa katika mazoezi ya mwisho jana katika Uwanja wa Taifa.Picha na Zainab Nyamka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad