HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, February 5, 2017

MAHAKAMA YATENGUA AMRI YAKE RAIS TRUMP

Jaji mmoja wa Marekani amesimamisha kwa muda utekelezaji wa amri ya Rais Donald Trump ya kuwazuia raia kutoka mataifa saba, yaliyo na raia wengi wa imani ya Kiislamu kuingia nchini Marekani.

Jaji wa Seattle alipuuzilia mbali sababu zilizotolewa na mawakili wa Serikali na kusema kuwa amri hiyo inaweza kusimamishwa mara moja huku kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa mahakamani.

Serikali inatarajiwa kukata rufaa ya dharura dhidi ya uamuzi huo wa mahakama, ambao ni changa moto kubwa kwa utawala wa Trump.

Serikali ya Marekani inasema kuwa makumi ya maelfu ya visa zimefutiliwa mbali tangu rais Trump kutia sahihi amri ya kupunguza idadi ya watu wanaopaswa kuingia nchini Marekani juma lililopita.

Kutokana na hatua hiyo, Idara ya Forodha ya Marekani imeyaambia mashirika ya ndege kwamba waruhusu abiria kupanda ndege kuelekea Marekani abiria ambao walinyimwa ruhusa baada ya Rais Trump kutoa amri kwamba watu kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi, wakataliwe kuingia Marekani.

Wakati huohuo waziri Mkuu wa zamani wa Norway, Kjell Magne Bondovik, alisema kuwa alizuiwa katika uwanja mmoja wa ndege mapema juma hili, katika tukio alilosema ni la uchokozi, kwa sababu eti alikuwa na visa ya Iran katika paspoti yake.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad