Mtaa Kwa Mtaa Blog

KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI CHAPOKEA MSAADA WA VIFAA VYA KUZUIA VUMBI KWA ASKARI

 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akipokea vifaa vya kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani  kutoka kwa msamaria mwema, Tahir Othman (kulia) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia askari  kuepukana na vumbi kuingia kwenye njia ya hewa  wawapo katika shughuli zao.Anayeshuhudia katikati ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Hamad Masauni.Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akionyesha kwa waandishi wa habari  jinsi ya kuvaa kifaa cha  kuzuia vumbi kwa askari wa usalama barabarani  alivyopokea kutoka kwa msamaria mwema,Tahir Othman(hayupo pichani) ,aliyejitolea vifaa hivyo ili kusaidia askari  kuepukana na  vumbi kuingia kwenye njia ya hewa wawapo katika shughuli zao.Kushoto ni  Naibu Waziri wa Wizara ya  Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mhandisi Hamad Masauni. Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri, jijini Dar es Salaam. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Wizara  ya Mambo ya Ndani ya Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani,Mhandisi Hamad Masauni, akiangalia jinsi ya kuvaa kifaa cha kuzuia vumbi kwa askari kutoka kwa Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga,ambae pia ni Katibu Mtendaji wa baraza hilo.Vifaa hivyo vilitolewa na msamaria mwema,Tahir Othman(hayupo pichani).Makabidhiano hayo yamefanyika ofisini kwa Naibu Waziri,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget