HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 23 February 2017

JOH MAKINI,DONGO JANJA KUPAMBA KILI MARATHON 2017

Wasanii Joh Makini na Dogo Janja wanatarajiwa kutoa burudani ya nguvu katika mbio za Kilimanjaro Marathon 2017 zinatarajiwa kufanyika Februari 26, Mkoani Kilimanjaro.

Akizngumza Mjini Moshi, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli aliwataka wakaziwa Moshi kujitokeza kwa wingi katika mbio hizo ambazo ndio kubwa Tanzania kwa sasa.

“Wasanii hawa wawili wanakubalika Moshi na tuna uhakika wakazi wa Moshi na wangeni wengine kutoka sehemumbalimbali watapata burudani ya aina yake mara baada yam bio hizi kukamilika siku ya Jumapili,” alisema nakuongeza kuwa burudani hii itaenda sambamba na Kilimanjaro Premium Lager za baridi za chupa zenye ujazo wa 375ml ambazo zinauzwa Tsh 2000.

“Hii ni chupa mpya ambayo kwa sasa tunaiuza Moshina Arusha na tuna uhakika wateja wetu watafurahia,” alisema.

Akizungumza, msanii Joh Makini alisema amejiandaa vizuri kukonga nyoyo za mashabiki wake na kuwataka wakazi wa Moshi wajitokeze kwa wingikushuhudiamuziki wa aina yake.

“Moshi ni nyumbani na nina uhakika mbioza Kilimanjaro marathon mwaka huu zitakuwa za aina yake kwani maandalizi  ni mazuri na tayari tunahisi jotolake Moshi,” alisema.

Naye Dogo Janja alisema, “Kati ya mikoa ambayo ina muamko mkubwa ni Kilimanjaro na ni faraja kutumbuiza katika hadhara kama hii ya watu kutoka pembe mbalimbali wanaokuja kushiriki Kilimanjaro Marathon 2017.”

Wakati huo huo usajili Mjini Moshi umeshaanza huku wakaziwa Moshi na wageni kutoka sehemu mbalimbali wakijitokeza kujisajili huku zikiwa zimebakizsiku mbili tu kabla yam bio hizo ambazo zitafanyika katika viwanja vya Chuo Cha Ushirika Moshi Jumapili Februari26 kuanzia saa kumi na mbili asubuhi.

Wadhamini wa mbio za mwaka huu ni Kilimanjaro Premium Lager-42km, Tigo 21km, GAPCO 10 km-walemavu, Grand Malt-5km. Wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair, Keys Hotel and new sponsors Anglo Gold Ashanti na KNAUF Gypsum.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad