HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 22, 2017

HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM YAPITISHA BAJETI YA SH. BILIONI 20

Na  Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imepitisha bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 ya bilioni 20 kutoka bajeti ya shilingi bilioni saba ya mwaka wa fedha 2015/2016.
Wajumbe wa baraza la jiji wamepitisha bajeti hiyo kwa kauli moja na kutaka kufikiria katika uwekezaji wa miradi mikubwa ili kufanana na majiji mengine duniani yenye ukubwa kama jiji la Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es  Salaam, Chacha Mwita amesema kuwa bajeti ya mwaka wa fedha 2017/2018 imeweka kipaumbele katika kulifanya jiji la Dar es Salaam kuwa la mfano katika usafi.
Amesema katika maeneo walioangalia ni kuongeza dampo katika manispaa za Kinondoni na Ubungo ili kuondoa usafirishaji wa taka hadi Pugu Kinyamwezi pamoja na ujenzi wa vyoo katika kila maeneo ambayo yana msongamano wa watu.
Mwita amesema kuwa lazima wajumbe wa baraza kuumiza kichwa katika miradi yenye manufaa kwa jiji katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Aidha amesema kuwa mradi wa DDC utaingizia mapato jiji shilingi milioni 750 kutoka shilingi Milioni 50 kwa mwaka wa fedha uliopita kutokana mazingira yaliyokuwepo kwa wafanyabiashara kulipa milioni 36 kwa chumba kwa mtu mwingine ambaye jiji inakuja kupata milioni sita kwa mwaka.
Akichangia katika baraza diwani  wa Mwananyamala, Songoro Mnyonge amesema kuwa vipaumbele vilivyowekwa vifanyiwe kazi katika kuleta mabadiliko katika jiji la Dar es Salaam.
Amesema katika mradi wa kutafuta eneo la makaburi katika kuweza kuwahifadhi ndugu zetu pamoja na manispaa  ya zingine kufanya hivyo kutokana na maeneo yaliyopo kujaa.
Wajumbe wa Baraza la Madiwa wa jiji la Dar es Salaam  wakiwa katika kikao cha bajeti leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad