HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 9 February 2017

GWAJIMA AWAKA KUTAJWA KATIKA ORODHA YA WANAOJIHUSISHA DAWA ZA KULEVYA

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima amesema kuwa ameokoka na anamtumikia mungu hivyo kutajwa katika orodha ya wanaojihusisha na dawa za kulevya iliyotangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni jambo ovu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Askofu  Gwajima amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam anafanya kazi vizuri lakini suala la kiutawala hawezi na kumuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli ambadilishie kazi.
Amesema yeye alikuwa Mpwapwa  katika kazi zake aliposikia kutajwa kwa jina lake na kumlazimu arudi na kuwasili pale alipoitwa bila kusubiri siku iliyopangwa ya kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Askofu  Gwajima amesema kuwa kuhusu mali anazomiliki ni kutokana na kazi anazofanya ikiwa kuwa na kampuni mbalimbali pamoja na kufundisha masuala ya farsasafa nje nchi na kulipwa dola za kimarekani 1000 kwa saa.
Aidha amesema kuwa kulindwa kwake ni kutokana na kuwa na usalama wake hata papa ana gari ambayo haipiti risasi wakati ni mtakatifu.
Askofu Gwajima amesema Makonda anachuki na wivu dhidi yake ndio maana anamhusisha na jambo ovu ambalo linamchafu mbele ya mungu.
Amesema kuwa yuko radhi kukaa ndani miaka 40 kutokana na kupigania suala la uovu ni jambo halitawe za kuvumiliwa.
 Askofu  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima akizungumza na waandishi wa habari juu ya  kutajwa kwao kujihusisha na dawa za kulevya leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
 Katibu Mkuu wa Kanisa  la Ufufuo na Uzima, Gwandu Mwangasa akizungumza na waandishi wa habari juu watavyopambana na katika kupigania Askofu wake Josephat Gwajima leo jijini Dar es Salaam.
 Asikofu  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima akitoka katika mkuna na kuelekea kituo  Kikuu cha polisi leo jijini Dar es Salaam.
Asikofu  wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima akiagana na waumini wa kanisa hilo leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad