HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 4 February 2017

AGHA KHAN YAADHIMISHA SIKU YA SARATANI KWA KUCHANGIA DAMU

 Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
HOSPITALI  ya  Agha Khan kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa Damu Salama katika kuadhimishia siku ya saratani duniani wameendesha uchangiaji damu kwa ajili kuokoa wgonjwa wa saratani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, wakati wa uchangiaji Damu katika Hospitali ya Agha Khan, Daktari wa Hospitali hiyo, Omary Sharman amesema katika kuadhimisha siku hiyo wamelenga kupata chupa 100.
Amesema kuwa saratani inahitaji kuwa na damu ya kutosha kutokana wagojwa kuhitaji damu kila wakati hivyo jamii ijenge mazoea ya kuchangia damu katika kuokoa wagonjwa  wa saratani pamoja wagonjwa wengine wasio na saratani.
Nae Meneja wa Masoko na Mawasiliano wa hospitali hiyo Olayce Lotha amesema kuwa damu inahitajika kwa kiwango kikubwa katika kuokoa wagonjwa wenye mahitaji ya kuongezewa damu.
Amesema Hospitali ya Agha Khan imekuwa ikifanya vipimo vya saratani ya matiti kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi bure  hivyo wanawake wanaaswa kufanya vipimo  katika hospitali ya Agha Khan.
Nae Afisa Uhamasishaji wa mpango wa Taifa wa Damu Salaama, Fatuma Mjungu amesema kuongezeka kwa wagonjwa wa saratani ndio kuongezeka kwa uhitaji wa damu katika kuokoa maisha yao.
Amesema jamii inawajibu wa kujitokeza katika uchangiaji damu kutokana na uhitaji watu wenye matatizo mbalimbali na kupona kwao kunahitaji kupata damu.
 Daktari wa Hospitali ya Agha Khan, Omary Sharman akiteta jambo na mchangiaji damu ,Sreejith Menon leo katika maadhimisho ya siku saratani duniani leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka,Glob ya jamii.
 Afisa Uhamasishaji wa Mpango wa Taifa wa Damu Salaama, Fatuma Mjungu akizungumza na Michuzi Blog juu ya wananchi kuchangia damu ili kuokoa wagonjwa wenye mahitaji  leo  jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Masoko na Mawasiliano waHospitali  ya Agha  Khan Olayce Lotha akizungumza Michuzi Blog juu wanawake kujitokeza kupima saratani kila jumamosi ya Mwisho wa mwezi bure katika hospitali  hiyo.
Sehemu ya wachangiaji damu wakiwa katika vitanda leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad