Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
TAASISI ya Karimjee Jevanjee imetoa ufadhili kwa wanafunzi wawili wanaokwenda kushuhudia tafiti mbalimbaliza kisayansi zinazofanywa na wanafunzi wa Dublin nchini Ireland.
Wanafunzi wawili hao walishinda katika mashindano ya wanasayansi chipukizi yaliyofanyika Agasti mwaka jana ambayo yaliratibiwa na Young Scientist Tanzania (YST).
Walioshinda mashindano hayo ni wasichana wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mtwara ambao ni Diana Sosoka pamoja na Nadhira Mresa.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Karimjee Jivanjee Foundation, Yusuf Karimjee amesema wanatoa ufadhili huo kwa kutambua mapinduzi ya uchumi yanahitaji wanasayansi.
Amesema kushuhudia mashindano ya tafiti za Sayansi itawaongezea kuboresha miradi yao walioifanya katika mashindano walioyafanya Agasti mwaka jana.
Yusuf amesema wanafunzi hao watapata ufadhili wa masomo ya elimu ya juu pindi watakapohitimu kidato cha sita.
Nae Mkurugenzi wa Young Scientist Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha amesema mashindano hayo ambayo yamekuwa kichocheo kwa wanafunzi kusoma masomo ya Sayansi na kuonyesha kwa vitendo.
Kamugisha amesema wanafunzi hao wataporudi watakuwa wameongeza ujunzi kupitia kwa wanasayansi wataokutana nao.
Mkurugenzi wa Young Scientist Tanzania (YST) Dk. Gosbert Kamugisha akizungumza na waandishi wa habari wakati utoaji wa zawadi na Ufadhili wa masomo kwa wanafunzi walioshinada mashindano ya Young Scientist iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa Karimjee Jivanjee Foundation, Yusuf Karimjee akimkabidhi zawadi Nadhira Mresa iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wakiwa na zawadi zao walizokabidhiwa kw ajili ya safari nchini Ireland iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment