HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 19, 2017

RAIS WA FIFA INFANTINO ATAKA SHERIA ZA SOKA KUBADILISHWA

Rais mpya wa FIFA Gianni Infantino anaonekana kutaka kubadili soka kabisa kwa kutaka kuondoa kila kitu cha Sepp Blatter na kuleta vyake hasa baada ya kupelekea mapendekezo ya kuongeza timu zitakazoshiriki kombe la dunia 2026 kufikia timu 48 na sasa amekuja na mpya ya kutaka kubadili namba ya kupiga penati.

Kwa kumtumia mkurugenzi wa mambo ya ufundi wa FIFA Marco Van Basten wamependekeza baadhi ya sheria mpya katika soka.
Kuondoa offside.

Akihojiwa na gazeti la Ujerumani liitwalo Bild,Van Basten amesema wanawaza kuondoa mchezo wa kuzidi katika soka.Alisema “sipati picha soka isipokuwa na ofside,washambuliaji watapata nafasi nyingi sana za kufunga”.Van Basten alisema mpira wa miguu utakuwa wakuvutia sana kama offside itaondolewa na anaamini jambo hilo litawafurahisha mashabiki na washambuliaji.

Kingine ni kubadili upigaji wa penati, Van Basten pia anaona kuna haja kubwa kwa FIFA kubadili aina ya upigaji wa penati na adhabu ya penati mchezaji ambapo upigaji wa penati ni mita kadhaa karibu na goli na kuupiga lakini sheria mpya anataka mpiga penati auweke mpira mita 25 kabla ya goli na kama anaweza atembee nao kuelekea golini kwa muda usiozidi sekunde nane.Aina hii ya upigaji penati sio ngeni kwani mwaka 1999 ilishafanyiwa majaribio nchini Marekani.

Kupunguza adhabu mipira ya kushika, Van Basten anaona kama adhabu ya kadi nyekundu ni kali mno kwa tukio hilo na  wanaliona kama tukio dogo lisilohitaji adhabu hiyo na wanazani inapaswa ipunguzwe kusitolewe kadi nyekundu mpira ukishikwa. Adhabu kam ile ya tukio la Luis Suarez mwaka 2010 wakicheza dhidi ya Ghana aliposhika mpira wakati ukiingia golini na kutaka ibadilishwe na kuwa ya njano.

Kapteni awe mtu pekee kuongea na mwamuzi, kama katika Rugby ni kapteni tu anayeongea na mwamuzi,asiruhusiwe mtu yeyote,mchezaji yeyote kuongea na mwamuzi.
Aina  ya faulo ya mchezo wa kikapu pale mchezaji anapocheza madhambi matano anatakiwa atoke uwanjani na  sasa Van Basten anaamini staili hiyo inapaswa kuletwa katika soka.

Kupunguza idadi ya mechi, hii itafurahiwa sana na makocha wageni Uingereza. Alianza Van Gaal akaja Jurgen Klopp walilalamikia idadi ya mechi kuwa nyingi Epl.Van Basten anataka idadi ya mechi zipunguzwe kutoka mechi 80 kwa msimu hadi 50 kwa msimu.

Kuongeza idadi ya Substitution.Van Basten anatamani kuongeza idadi ya wachezaji wa sub kuanzia 5-7,kwa muda mrefu wadau wa soka wamekuwa wakizungumzia kuhusu suala la kuongeza wachezaji wa akiba na sasa FIFA inatarajia kuliangalia suala hili.

Kuzifanya dakika 10 za mwisho kutumika ipasavyo.”Tunajua kutokana na kuongeza idadi ya wachezaji wa akiba pamoja na aina ya upigaji penati vitachukua mda mrefu uwanjani na itatubidi kuhakikisha dakika 10 za mwisho zinatumika kiuhakika” Van Basten alisema watahakikisha hakuna upotezaji muda katika dakika zamwisho za mchezo.

Hayo ni mapendekezo tu kutoka kwa mkurugenzi wa ufundi wa FIFA na  sasa atawasilisha mapendekezo hayo katika kamati ya FIFA yaweze kujadiliwa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad