HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, January 22, 2017

RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI MHE, ALHAJ ALI HASSAN MWINYI AMEWATAKA WATANZANIA KUWA NA TABIA YA KUENDELEZA YALIYO MEMA.

Na Emanuel Masaka, Globu ya Jamii
Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Alhaj Ali Hassan Mwinyi amewataka watanzania kuwa na tabia ya kuyafanyia muendelezo yale mema wanayoyafanya, kama walivyofanya kampuni ya NIDA TEXTTILES kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya kiongozi wa waislamu Mtume Muhammad (S.A.W).


Akizungumza katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam Al-Haji Mwinyi amesema kua Mtume Muhammad alikuwa akifunga kila siku ya Jumatatu ikiwa ni ishara ya kusherekea siku aliyozaliwa.

Hivyo ni vyema kuiga mfano huo wa kufanya matendo mema kwa kuyarudia mara kwa mara na kuyadumisha, huku akipongeza uongozi wa NIDA kwa kuwaalika na kusherekea pamoja kwani amejifunza mengi kupitia mawaidha yaliyotolewa na viongozi wa dini waliohutubia akiwemo Sheikh Ally Basaleh.

Sherehe hizo zimepambwa kwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali akiwemo Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Gharib Bilal, Naibu Waziri Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Suleiman Jafo, Naibu Waziri Wizara ya Afya Hamis Kigwangala, Waziri wa zamani wa Ulinzi Profesa Juma Kapuya, Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba, Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega huku kwa viongozi wa dini walikuwepo Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum na Kadhi Mkuu wa Tanzania Abdallah Mnyaa ambapo wote kwa pamoja walipewa zawadi maalum na kampuni hiyo.

 Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza na viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali juu ya watanzania kuyafanyia muendelezo wa yale mema kama walivyofanya kampuni ya NIDA TEXTTILES kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya kiongozi wa waislamu Mtume Muhammad (S.A.W). leo jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib  Bilal, akizungumza na  viongozi mbalimbali wa Dini na Serikali katika kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya kiongozi wa waislamu Mtume Muhammad (S.A.W). leo jijini Dar es Salaam.
 Shehe Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam,Sheikh Alhadi Mussa Salim akizungumza machache katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Dk. Hamisi Kigwangalla leo jijini Dar es Salaam. 
 .Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib akisalimiana na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Seleman Jaffo leo jijini Dar es Salaam.


.Sehemu ya viongozi mbalimbali wa dini wakiwa katika hafla hiyo ya Maulid iliyofanyika jijini Dar es Salaam.


Waislamu waliojitokeza katika   kusherekea kumbukumbu ya mazazi ya kiongozi wa waislamu Mtume Muhammad (S.A.W). yaliyofanyika Leo Jijini Dar esa salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad