Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza katika mkutano wa Wadau wa Afya uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Meru,kushoto ni Mganga Mkuu wa mkoa,Dk frida Mokiti.
Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dokta Frida Mokiti amesema kuwa uhaba wa
vituo vya afya katika maeneo ya pembezoni mwa miji umekua ukichangia vifo vya
mama wajawazito na watoto kutokana na kutembea umbali mrefu kutafuta huduma
hiyo.
Akizungumza katika Kikao kazi cha Mkoa kinachojadili hali ya afya ya mkoa, Dr.
Mokiti amesema kuwa juhudi za makusudi zinahitajika kuhakikisha kuwa huduma
za afya kwa mama na mtoto zinapatikana kwa urahisi ili kupunguza tatizo hilo
ambalo limekua likirudisha nyuma afya ya wakina mama pamoja na kukatisha
maisha yao.
Akizungumza katika Kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Gambo amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kuhakikisha kuwa
wanajenga Kituo cha Afya katika kila tarafa ili kusogeza karibu huduma za afya
kwa wananchi pia amewataka viongozi kuweka mipaka katika maeneo ya zahanati
ili kuepuka uvamizi wa maeneo hayo yanayowahudumia watu.
“Wakati sasa umefika wa kuhakikisha tunatokomeza kabisa changamoto hii ya
vifo vya mama na mtoto, inasikitisha sana kuona mama anafariki wakati wa
kujifungua kwa sababu tu amekosa huduma ya afya karibu na makazi yake,lazima
tuwalinde na kuwajali wananwake, kwa sababu bila ya wao kujifungua hata sisi
tusingekuwepo” Alisema Gambo.
Aliongeza kuwa Kila Halmashauri ihakikishe inatenga Fedha kwenye mapato yake
ya ndani halkadhalika Ruzuku toka Serikali Kuu ielekezwe kwenye Miradi ya
Afya na tuendelee kutafuta wadau watakaotusaidia katika utekelezaji wa miradi hii
bila kusahau uhamasishaji wa nguvu za wananchi kwa Pamoja tutatokomeza tatizo
hili.
Kwa upande wake Mkazi wa Arusha Hussein Igunge na Mkuu wa Wilaya ya
Longido Mhe. Daniel Chongolo wameitaka serikali iboreshe huduma za afya
ikiwemo upatikanaji wa madawa kwa wale waliokata bima ili waweze kunufaika
na bima zao pamoja na uhaba wa watumishi katika sekta ya afya.
Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha,Dk Frida Mokiti akizungumza katika mkutano wa Wadau wa Afya uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Meru,kulia ni Mkuu wa mkoa,Mrisho Gambo akimsikiliza kwa makini,kushoto ni Katibu Tawala wa wilaya ya Karatu na Katibu Tawala mkoa wa Arusha,Richard Kwitega.
Baadhi ya Watalaam wa sekta ya afya wakiwa kwenye mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Meru mkoa wa Arusha.
Baadhi ya viongozi wa dini walioshiriki mkutano huo wakisikiliza kwa makini pia waliahidi kushirikiana na mfuko wa Bima ya Afya(NHIF)kuhamasisha waumini wao kujiunga na mfuko wa CHF.
Wakuu wa wilaya za mkoa wa Arusha wakiwa kwenye mkutano huo uliojadili kwa kina mikakati ya kuinua sekta ya Afya kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Arusha,Gabriel Daqarro,Mkuu wa wilaya ya Monduli,Idd Kimanta na Mkuu wa wilaya ya Karatu,Theresia Mahongo.






No comments:
Post a Comment