HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 29 January 2017

MICHUANO YA ULEGA CUP YAENDELEA LEO MKOANI PWANI

Mashindano ya Ulega cup yameendelea hii leo katika kiwanja cha Mwalusembe ambapo imezikutanisha timu ya Mkamba FC na Mwalusembe FC.

Timu ya Mkamba ndio ilikuwa ya kwanza kuandika gori la kwanza Dakika ya 20 kipindi cha kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Juma Mbondo na katika kipindi cha pili Mwalusembe fc walirudisha gori katika Dakika ya 12 kipindi cha pili kupitia kwa kiungo mchezeshaji Saidi kwepu .

Mpaka refa Samson Mwita anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalibaki Mwalusembe 1 na Mkamba 1. 

Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mkuranga Abdallah Ulega ,amewataka vijana kutokata tamaa katika mchezo wa mpira kwani michezo huo ni ajira.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wachezaji wa timu za Mkamba na Mwalusembe fc katika kituo cha Mwalusembe leo mkoani Pwani.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Mwalusembe fc leo mkoani Pwani.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Mkamba leo mkoani Pwani.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Mchezo ukiendelea ambambo timu zote zimetoka sale ya goli moja moja.
.Kamanda wa ulinzi katika mashindano ya Ulega Cup akiwadhibiti mashabiki waliokuwa wakileta fujo wakati wa mechi kati ya Mkamba FC na Mwalusembe FC leo Mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad