HABARI MPYA

Home Top Ad



Post Top Ad

Sunday, 29 January 2017

MATUKIO KATIKA PICHA: YANGA YAICHABANGA MWADUI FC BAO 2-0 UWANJA WA TAIFA LEO

Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara, Yanga wamefanikiwa kukaa kileleni mwa msimamo wa  ligi baada ya kutoka na ushindi wa goli 2-0 kwenye mchezo uliofanyika leo katika dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Obrey Chirwa aliyeingia dakika ya 62 akichukua nafasi ya Haruna Niyonzima alikuwa nyota wa mchezo huo kwa kuifungia timu yake goli 2 katika dakika ya 69 na 82.

Yanga waliingia uwanjani wakitafuta ushindi wa aina yoyote ambapo mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika timu  hizo zilienda mapumziko wakiwa hawajafungana.

Mwadui waliokuwa makini katika safu yao ya ulinzi waliweza kuwadhibiti washambuliaji wa Yanga na kuwafanya kushindwa kupata goli la mapema.

Kila upande walifanya mabadiliko kwa ajili ya kusaka ushindi huo, na baada ya matokeo haya Yanga anaongoza ligi akiwa na alama 46, akifuatiwa na Simba mwenye alama 45 huku Azam akiwa na alama 34.
 Wachezaji wa Timu ya Mwadui, wakiusindikiza mpira kwa macho wakati ukiingia wavuni, baada ya kupigwa kwa umaridadi mkubwa na Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa na kuipatia timu yake goli la kuongoza.
 Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa na Simon Msuva wakishangilia ushindi wao dhidi ya Mwadui Fc, katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara, uliopigwa jioni hii katika Dimba la Taifa, jijini Dar es salaam. Yanga imeshinda 2-0.
 Furaha ya ushindi kwa wachezaji wa Yanga.
 Mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe akiwania mpira na Beki wa Mwadui, Nassor Chollo, wakati wa mchezo wa Ligi kuu Tanzania bara, uliopigwa katika Dimba la Taifa, jijini Dar es salaam leo. Yanga imeshinda goli 2-0.
  Mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa kwa mara ya pili akiipatia timu yake goli dhidi ya Mwadui.











No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad