HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 28, 2017

MATUKIO KATIKA PICHA: SIMBA YACHEZEA KICHAPO CHA BAO 1-0 TOKA KWA AZAM, UWANJA WA TAIFA LEO

TIMU ya soka ya Azam imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Simba katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.

Mchezo huo ulioanza kwa kila upande kucheza kwa umakini na kutafuta goli la ushindi uliweza kudumu kwa takriban dakika 45 bila timu hizo kufungana.

Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kufanya mabadiliko ya kumtoa Mchezaji wake Mzamiru Yassin na kuingia Shiza Kichuya ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji, baadae akaingia  Ibrahim Ajib akichukua nafasi ya Janvier Bukungu aliyeumia.

Mnamo dakika ya 70 ya mchezo, John Bocco akitumia udhaifu wa beki Method Mwanjali aliweza kuifungia timu yake goli la kwanza na la ushindi ambalo lilidumu mpaka dakika 90 za mchezo.

Azam waliendelea kulisakama goli la Simba kutaka kutafuta goli la pili lakini kwa upande wa Simba nao waliendelea kusaka goli la kusawazisha na kufanya mchezo huo, kumalizika kwa ushindi wa goli 1-0 kwa upande wa Azam.

Baada ya matokeo haya, Simba inaendelea kusalia kileleni kwa alama 45, wakifuatiwa na Yanga wenye alama 43 wakiwa na mchezo mmoja mkononi na Azam wakipanda mpaka nafasi ya tatu kwa alama 34.
 Mshambuliaji wa Azam, John Bocco "Adebayor" akiachia shuti kali lililomshinda Kipa wa Simba, Daniel Agyei na kwenda moja kwa moja wavuni na kuipatia timu hiyo bao la ushindi lililodumu mpaka mwisho wa mchezo.
 Mshambuliaji wa Azam, John Bocco "Adebayor" akishangulia baada ya kuifungia timu yake bao la kuongoza na la ushindi.
 Wachezaji wa Azam wakifurahia ushindi wao.
 Beki wa Azam, Yakubu Mohammed akiwania mpira na Mshabuliaji wa Simba, Laudit Mavugo katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo. Azam imeshinda bao 1-0.
 Mzamiru Yassin akipimana msuli na kiungo wa Azam, Himid Mao kuhu Said Ndemla akimsaidia.
 Said Ndemla wa Simba akiondoka na mpira.














No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad