HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 24, 2017

Kilimanjaro Premium Lager yawataka washiriki kujisajili mapema Marathon

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli ambaye bia yake ndio mdhamini mkuu wa Kilimanjaro Marathon amewataka washiriki wa mbio hizokujisajili mapema ili kuepuka na msongamano dakika za mwisho.

Alitoa rai hiyo Jijini Dar es Salaam huku akisema mbio hizo zimekuwa kubwa na maarufu na hivi kuwavutia washiriki wengi  jambo ambalo linalazimu washiriki waanze kujisajili mapema.

“Mwaka jana kulikuwa na wakimbiaji zaidi ya 8000 kutoka nchi zaidi ya 45 na tunatarajia kupata washiriki wengi zaidi mwaka huu,” alisema na kuongeza kuwa Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuwa mdhamini mkuukwa miaka 15 mfulululizo sasa.
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu Kilimanjaro Marathon 2017. Wengine mini mbio za kilometa 5, Meneja Masosko wa Grand Malt Tanzania kutoka kushoto ni Meneja wa Grand Malt, Oscar Shelukindo anayedhamini mbio za kilometa 5, Meneja Masoko wa GAPCO Tanzania Caroline Kakwezi-kilometa 10 kwa watu wenye ulemavu na Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Kaskazini, George Lugata-kilometa 21.

Alisema wakati wa msimu huu wa Kilimanjaro Marathon, Kilimanjaro Premium Lager itaanza kuuzwa katika chupa mpya yenye ujazo wa mililita 375 kwa Kilimanjaro na Arusha.

“Ni matumaini yetu kuwa washiriki wote na wengineambao watakuwa Moshi wakati huo watafurahia bia yao namba moja ya Kilimanjaro Premium Lager ikiwa kwenye chupa mpya ya mililita 375 na ya baridi baada ya kukimbia,” alisema.

Kwa upande wake Meneja wa Grand Malt, Oscar Shelukindo ambaye anadhamini mbio za kilometa 5 alisema mipango yote imekamilika na kusisitiza kuwa watu 4000 wa kwanza kujisajili katika mbio za kilometa 5 watapata fulana za Grand Malt.

Alisema Grand Malt zenye kopo na chupa zenye muonekano mpya zitauzwa kwa wingi na pia kutolewa kama zawadi. “ Hizi ni mbio zinazohusu watu wa rika mbalimbali hivyo Grand Malt ndio kinywaji sahihi  cha kuwaongezea nguvu wanapokimbia,” alisema.

Mkurugenzi Mtendaji wa Executive Solutions, Aggrey Marealle ambaye kampuni yake ni mratibu mkuu wa Kilimanjaro Marathon inayoandaliwa na Wild Frontiers alisema maandalizi ya mwaka huu yamekamilika na wanatarajia mbio hizi zitakuwa kubwa zaidi za za kusisimua.

Alisema kwa mara ya kwanza usajili utafanyika Dar es Salaam katika viwanja vya Mlimani City  kuanzia Februari 18 hadi 19 kisha Arusha-Kibo Palace Hotel na kumalizikia Moshi-Keys Hotel kabla ya mbio hizo kufanyika Februari 26 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU).

“Safari hii waandaaji wataweka vyoo kadhaa kaika njia wanayopita wakimbiaji, jamoambalo halikuwahi kufanyika miaka ya nyuma,” alisema.

Wadhamini wengine ni pamoja na Tigo 21km, GAPCO 10 kmkwa watu wenye ulemavu. Wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair, Keys Hotel and new sponsors Anglo Gold Ashanti and KNAUF Gypsum.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad