HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 21, 2017

Huawei, Skytel wazindua duka kubwa Arusha

Afisa Biashara wa jiji la Arusha, Steven Sultan(wa pili kulia) na Meneja wa Huawei jijini Arusha,Qin Yilin(wapili kushoto) wakikata utepe kuashilia uzinduzi wa duka la Huawei Skytel uliofanyika jana jijini Arusha.Kuhoto ni Meneja Huawei Kanda Kanda ya Kaskazini, Betrice Vitalis.
Afisa Biashara wa jiji la Arusha, Steven Sultan(wa pili kulia) na Meneja wa Huawei jijini Arusha,Qin Yilin(wapili kushoto) wakipongezana kwa kushikana mikono mara baada ya kukata utepe kuashilia uzinduzi wa duka la Huawei Skytel uliofanyika jana jijini Arusha.Kuhoto ni Meneja Huawei Kanda Kanda ya Kaskazini, Betrice Vitalis.
Meneja Huawei Kanda Kanda ya Kaskazini, Betrice Vitalis(kushoto) akitoa maelekezo ya bidhaa za Huawei kwa fisa Biashara wa jiji la Arusha, Steven Sultan mara baada ya uzinduzi wa Duka ka Huawei Skytel kuzinduliwa rasmi jijini Arusha.Kulia ni Meneja wa Huawei jijini Arusha,Qin Yilin na Mkurugenzi wa Duka hilo, Bobkevin Shoo.

Kampuni ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Huawei Tanzania kwa kushirikiana na Mfanyabiashara maarufu wa simu jijini Arusha, Skytel wamefungua duka kubwa liitwalo “ Huawei Skytel Brand Shop” katika Jiji la Arusha. Hatua hiyo ni mwendelezo wa Huawei katika kutekeleza moja ya mikakati yake ya kujitanua kibiashara nchini.

Huawei imeona kuwepo wa Duka hili kubwa la Skytel, katika Jiji la Arusha kunatokana na kukua mahitaji ya bidhaa za Huawei nchini na hivyo kutoa fursa ya watumiaji kupata huduma kwa karibu zaidi.

“Tunafahamu watanzania walio wengi wanachohitaji, ndiyo maana leo hii tuko Jijini Arusha. Tunaamini kuwa hii ni fursa pekee kwa wakazi wa Arusha na miji ya jirani kupata bidhaa zetu zenye ubora na viwango vya hali ya juu. Tunaamini kuwa Skytel wana jina kubwa katika Jiji la Arusha na hivyo itatusaidia sisi kutimiza lengo letu, alisema Meneja wa Huawei jijini Arusha,Qin Yilin.

Mwaka huu kampuni hii ya simu ilijipanga kusambaza huduma yao nchi nzima, sambamba na kufungua maduka kwaajili ya kusogeza huduma zetu kwa wateja. Hali hii imetuongezea wepesi wa utoaji wa huduma zao kwa kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kutambua mahitaji muhimu kwa wateja wetu,

Tanzania imefaidika na uhusiano mzuri uliopo kati yake na Huawei kwa kuwa na miradi mbalimbali yenye lengo la kuboresha teknolojia ya mawasiliano. Huawei inampango wa kukuza teknolojia ya mawasiliano nchini Tanzania na sasa imeanza kushirikiaba kwa karibu na wazawa kama Skytel. Milango iko wazi kwa yeyote anayetaka kutuunga mkono kiabiashara.

Wakati Huawei inazindua duka hilo katika Ukanda wa Kanda Kaskazini, Meneja wa Huawei Arusha alitangaza uwepo wa simu mpya ya kisasa, Huawei Y3II na nyinginezo, katika soko la simu nchini.

Alisema kuwa simu hiyo ina ubora na kuwataka watanzania kutumia, akifafanua zaidi kuwa ni simu yenye ubora, lakini gharama yake sio kubwa, ikilinganishwa na simu za makampuni mengine.Pia bidhaa nyingine zitaambatana na simu hiyo kama matoleo mangine tofauti Huawei P9, Y3c, Y5II ,Y6II, Y3lite na nyingine nyingi.

Hizi ndizo faida za kuwa na duka kubwa katika Jiji la Arusha. Kuanzia sasa wanunuzi wa bidhaa zetu wana fursa ya kupata bidhaa zetu zote kwa wakati. Tunaanza na simu hii ya Huawei Y3II ambayo kwa hakika kila atakayeamua kuitumia ataipenda kwa ubora wake.

Kwa mujibu wa Meneja huyo, Kampuni ya Huawei inaendelea na mchakato wake wa kusogeza huduma zake kwa wateja wake, kwa lengo la kutimiza malengo yake ili kupambana na soko la mawasiliano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad