
Rais wa shirikishola Soka Duniani 'Fifa'
Gianni Infantino
Shirikisho la Soka Duniani Fifa linatarajiwa kupiga kura leo kuamua kuhusu mpango wa kupanua Kombe la Dunia liwe linashirikisha mataifa 48. Mpango huo ukiidhinishwa, basi utaanza kutekelezwa Kombe la Dunia la 2026, na utakuwa na faida kwa nchi za Afrika na Asia.
Rais wa shirikisho hilo Gianni Infantino amekuwa akipiga debe mpango huo na amekuwa na uungwaji mkono mkubwa, pia anataka michuano hiyo iwe na makundi 16 ya mataifa matatu kila kundi na klabu mbili kutoka kila kundi zitafuzu kwa hatua ya mtoano na iwapo mpango huo utaidhinishwa, basi itakuwa mara ya kwanza kwa Kombe la Dunia kupanuliwa tangu mwaka 1998..
Kuna mapendekezo matano ambayo baraza kuu la Fifa lenye wanachama 37 litaangazia ikiwemo timu 48 na zikiwa kwenye makundi 16 na timu tatu kila kundi ambapo timu mbili bora zitasonga kwa hatua ya mtoano na kuingia timu 32 (mechi 80 kwa jumla).
Mapendekezo mengine ni kuwa na timu 40 na makundi 10 ya timu nne kila kundi ambapo mshindi, na timu sita pekee zinazomaliza nambari mbili kundini ndizo zinafuzu (mechi 76) nyingine ni kuwa na timu 40 na makundi manane ya timu tano kila kundi (mechi 88) kusalia na kuendelea kusalia na timu 32 .
Infantino, 46, ambaye alimrithi raia mwenzake Sepp Blatter kama rais wa Fifa mwezi Februari 2016 alifanya kampeni akiahidi kupanua michuano hiyo. Awali alipendekeza michuano ya timu 40, wazo lililowasilishwa na rais wa wakati huo wa Uefa Michel Platini 2013, kabla ya kubadilisha msimamo na kuunga mkono michuano ya timu 48.
Chini ya mpango wa Infantino anaoupendekeza kwa sasa, mechi zinaongezeka kutoka 64 hadi 80, lakini fainali bado zinaweza kuchezwa kwa kipindi sawa na cha sasa cha siku 32. Taifa halitatakiwa kucheza zaidi ya mechi saba, sawa na ilivyo chini ya mpango wa sasa na dhaifu pekee ni kwamba huenda mikwaju ya penalti ikatakiwa kutenganisha klabu zinazotoka sare kwenye makundi.
Historia ya Mabadiliko Kombe la Dunia
Kombe la DuniaTimu
1930 Uruguay 13
1934 Italy 16
1950 Brazil 13
1954 Switzerland 16
1958 Sweden 16
1974 West Germany 16
1982 Spain 24
1986 Mexico 24
1998 France 32
Kwa msaada wa BBC.
No comments:
Post a Comment