Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,
Wazee na watoto Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa siku siku 7 kwa Katibu Mkuu kumaliza changamoto
zinazoikumba hospitali ya Rufaa ya Kitete iliyopo mkoani Tabora.
Dkt. Kigwangalla ameyasema hayo alipofanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Rufaa ya Kitete Mkoani
Tabora na kukagua miradi ya chumba cha
upasuaji pamoja na Chuo cha AMOS
kilichopo mkoani humo .
“Chumba hiki cha upasuaji na Chuo vimekamilika mpaka thamani za ndani tangu
miaka miwili iliyopita Sababu ni kwamba Serikali yetu haikutoa counter-part
funding huku Benki ya Maendeleo ya Afrika ikiwa imetimiza ahadi yake kwa asilimia mia
moja”alisema Dkt. Kigwangalla.
Hata hivyo Dkt. Kigwangalla amesema kuwa
amefurahishwa kutekelezwa kwa baadhi ya maagizo aliyoyatoa kama vile kuondoa msongamano wa wagonjwa kwenye wodi za
wanawake wajawazito na watoto.
Kwa mujibu wa Dkt. Kigwangalla amesema kuwa
uongozi wa Hospitali hiyo umefanikiwa kuboresha huduma ya upatikanaji wa dawa zote
muhimu na huduma kwa wateja ikiwemo lugha nzuri kutoka kwa wahudumu imeboreshwa..
Aidha Dkt. Kigwangalla amesema anashukuru uongozi
wa Hospitali hiyo kwa kufanya ukarabati mkubwa wa majengo ya wodi za wagonjwa
na sasa hakuna tena msongamano na huduma zinatoka kwa wakati sahihi.
No comments:
Post a Comment