HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 7, 2016

WABUNIFU WA BIDHAA ZA KILIMO WAKUTANISHWA NA TASISI ZA FEDHA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Jumla ya Vikundi 16 kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini vinavyojiusisha na masuala ya kilimo vimeweza kukutanishwa na Tasisi za kifedha na mabenki hili waweze kuwezeshwa kama mpango wa taasisi ya Land O Lakes.

Akiazungumza na Globu hii Mshauri wa biashara bunifu kutoka tasisi hiyo ,Renalda Lema amesema kuwa katika vikundi hivyo 16 wameweza kuwakilishwa na watu wawili wawili hili waweze kuwasilisha ubunifu wao kwa taasisi hizo hili waweze kupata fursa ya kupanua biashara yao.

“umeweza kuona wabunifu walivyoweza kutengeza mashine mabalimbali ambazo zitaweza kumuondoa mkulima kutoka sehemu moja hadi nyingine hasa katika serikali hii ambayo inahamasisha uchumi wa viwanda hivyo sisi tumeona uchumi wa viwanda auwezi kufanikiwa bila ya kuanza kuwawezesha wakulima katika hatua ya mwanzo kabisa” amesema Renalda.

Ametoa wito kwa wadu na taasisi mbalimbali ambazo zinahitaji kuwawezesha wakulima hao kwa namna moja hama nyingine waweze kuwasiliana na taasisi ya Land O’ Lakes waweze kuwakutanisha na wakulima hao.
  Mkurugenzi wa tasisi ya fedha ya Brac, Mahufuzii Ashrafu , akizungumza na baadhi ya wabunifu waliiokutanishwa na kampuni hiyo ili waweze kuwezeshwa kama mpango wa tasisi ya  Land O Lakes ili waweze kufikia malengo waliyojiwekea.
 Mbunifu wa mashine ya kukamua matunda kutoka mkoa wa Songwe, Yohana Mwanzyunga(wa kwanza kulia) akiwaonyesha washiriki wengine mtambo wa kukamua matunda.
Baadhi ya washiriki wakiangalia mashine ya kupukucha halizeti

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad