Na Anthony John, Globu ya Jamii.
KATIBU Tawala wa Manispaa ya Ilala Edward Mpogolo amempongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kuwainua wanawake kwa kuwapa nafasi katika nyanja mbali mbali za Uongozi Wa kisiasa na utendaji Wa umma hapa nchini.
Akizungumza katika Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsiakwa mama na watoto Mkoa wa Ilala Mpogolo
amesema Rais Magufuli ameweza kuwainua wanawake na kuwa na imani nao hasa katikakazi za kiserikali na kuweza kuwapa uongozi wa juu kwenye sekta tofauti.
Akielezea ukatili wa kinjisia, Mpogolo amesema kutokana na taarifa zilizofanywa na Shirika la Afya Duniani inaonyesha kuwa Asilimia 15 Hadi 71 waliathirika na ukatili wa kimwili au wa kingono ulifanywa na wanaume au Wenzi wao utafiti ulibaini Pia zaidi ya Asilimia 90 ya waathirika wa ubakaji wanawafahamu wahalifu wao.
Pia aliwataka watoto Wanaoishi katika Wilaya ya Ilala kutokunyamazia vitendo mbali mbali vya ukatili wa kinsia unaofanywa dhidi Yao.
Hata Hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, ACP Salum Hamdani aliwataka wazazi na watoto kutokunyamazia ukatili wa kijinsia unaofanywa dhidi yao na badala yake kutoa taarifa katika vituo vya Polisi.
Katibu huyo alilishukuru Jeshi la polisi kwa kupitia kamanda wa mkoa wa kipolisi Ilala kwa maandalizi ya kampeni ya siku 16 Ya kupinga ukatili wa kijinsia.
Katibu Tawala wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala akiwa katika maadhimidho ya siku 16 ya kipinga ukatili wa kijinsia (kulia) Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala ACP, Salum Hamdan.
Baadhi ya wakazi wa Vingunguti waliojitokeza katika Madhimisho ya Siku 16 kupinga ukatili wa kijinsia.
No comments:
Post a Comment