HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 4, 2016

WAMAMA WAWILI WAKAMATWA LEO JIJINI ARUSHA WAKIIBA KWENYE DUKA LA NGUO


Picha ikionyesha wamama wawili ambao ni wezi waliokamatwa katika mtaa wa koni eletronic uliopo jijini Arusha wakiwa wanaiba katika duka moja la mfanyabiashara wa nguo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini wakiwa wamezingirwa na wananchi mara baada ya kukutwa wakiwa wanajidai wanataka kununua nguo kumbe wanachagua nguo na kuziweka katika mapochi yao makubwa waliyobeba ,wamama hawa waliambulia kipigo nusu wa chomwe moto lakini walibahatika kusaidiwa na polisi mara baada ya polisi kufika eneo la tukio na kuwachukuwa kisha kuwapeleka katika kituo cha polisi

            Na Woinde Shizza, Arusha

Kumekuwepo na tabia ya baadhi ya wamama ,wadada kuwa na tabia ya kuingia madukani na kuibia wafanya biashara wanguo pamoja na vipodozi vitu mbalimbali.

Hapo nyuma kumekuwepo na malalamiko mengi sana wanayotoa wafanyabiashara hawa kuwa wanakuwa wanaibiwa wengine ambao wamefunga kamera madukani mwao wamekuwa wakirusha picha zinazoonyesha video za wadada hao wakiwa wanaiba.


Hivi leo kuna kina mama wawili wamekamatwa katika mtaa wa koni eltronic ulipo ndani ya jijini Arusha wakiwa wanaiba katika duka la dada mmoja mfanyabiashara wanguo ,na inasemekana hao wamama walikuwa wamezoea kuiba katika duka hilo naweza kusema kuwa walipafanya kama shamba la bibi sasa leo hii wamekamatwa nusu wachomwe moto.

Mmiliki wa libeneke la kaskazini aliweza kuwashuhudia wamama hao wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi huku wakiwa wamezingirwa na wananchi wakiwa wanapigwa vibao na kuaambiwa wanazalilisha wanawake kwa kuwa wezi 

Wadada hao mara baada ya kukamatwa awali walisema wametokea nchini kenya lakini baadae walibadilika na kusema wametokea mkoani hapa hapa Arusha 

Wananchi wanye asira kali waliwapiga huku wengine wakitaka wachomwe moto ili kukomesha tabia hiyo lakini kabla ya tukio la uchomaji moto kutokea ndipo askari polisi walitokea na kuwachukuwa kisha kuwapeleka kituo cha polisi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad