HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 25, 2016

WALIMU WASTAAFU NCHINI WAANZISHA JUKWAA

 Mwenyekiti wa Jukwaa la  Wastaafu wa Taaluma ya Elimu, Profesa Herme Joseph Mosha akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wakati wa kukitambulisha rasmi Jukwaa hilo katika Ukumbi wa Idara ya Habari –MAELEZO leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho Bibi. Khadija Mchatta Maggid na Muhwela Kalinga.
 Katibu Mtendaji wa Jukwaa la Wastaafu wa Taaluma ya Elimu, Bibi. Marystella Maufi Wassena akifafanua jambo wakati wa mkutano wa kukitambulisha Jukwaa hilo leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Profesa. Herme Joseph Mosha
 Mjumbe wa Sektretarieti ya Jukwaa la  Wastaafu wa Taaluma ya Elimu Bw. Muhwela Kalinga akielezea jambo wakati wa mkutano wa kukitambulisha chama hicho leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa hilo Profesa Herme Joseph Mosha.
 Baadhi ya Sekretarieti ya Jukwaa la  Wastaafu wa Taaluma ya Elimu wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Picha zote na: Frank Shija

WALIMU wastaafu nchini wameanzisha jukwaa maalum litakalotumika kwa ajili ya kushauriana na kubadiliana uzoefu baina yao na serikali kuhusu mfumo na utaratibu utoaji bora wa elimu nchini.
Hayo yamesemwa leo, Jijini Dar es Salaam na mwenyekiti wa jukwaa hilo Prof. Herme Mosha alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya lengo la uanzishwaji wa jukwaa hilo.
Prof. Mosha alisema walimu wastaafu wana uzoefu mkubwa katika sekta ya elimu hivyo kupitia jukwaa hilo watakuwa wakitafakari maeneo ambayo sekta ya elimu  haitoweza kufanya vizuri na hivyo kuishauri hatua zinazopaswa kuchuliwa na Serikali.
“Unapokuwa mtumishi wa Umma unaona kila kitu kinaenda sawa, lakini unapokuwa nje unaona kuna mambo mengi ambayo yalikuwa hayaendi sawasawa,” alifafanua Prof. Mosha.
Kwa mujibu wa Prof. Mosha alisema alipokuwa katika utumishi Umma walikuwa wakiandikisha wanafunzi wa darasa la kwanza  kwa asilimia 95, lakini baada ya tamko la elimu bila ada idadi ya wanafunzi iliongezeka zaidi.
Prof. Mosha alisema kitendo hicho kinaonyesha kuwa n kwamba  asilimia kubwa ya watoto walikuwa hawaandikishwi kuanza elimu ya msingi kutokana na vikwazo vya ada.
Aidha aliipongeza serikali Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuboresha sekta ya elimu ambapo kwa sasa kila mwanafunzi anakaa katika dawati tofauti na miaka ya nyuma.
Kwa upande wake Katibu wa Jukwaa hilo Bi. Marystella Wassena alisema jukwaa hilo litakuwa likijishughulisha pia na kufanya tafiti  mbalimbali za kuboresha sekta ya elimu.

Bi. Wassena aliwataka walimu waastaafu nchini kujiunga na jukwaa hilo na kutumia uzoefu walioupata ili kuishauri Serikali na kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa katika ngazi zote za elimu. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad