HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 12, 2016

UUZAJI HOLELA WA MAENEO YA WAZI JIJINI ARUSHA WAWALIZA WANANCHI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akizindua daraja ambalo limejengwa na wawekezaji lililogarimu zaidi ya shilingi milioni 65 za kitanzania

Na Woinde Shizza,Arusha.


Wananchi wa Kata ya Engutoto jijini Arusha wamelalamikia uuzaji holela wa maeneo ya wazi ya serikali hali inayopelekea uhaba wa maeneo ya kujenga huduma za kijamii kama zahanati na shule ambazo hazipatikani katika kata hiyo, hivyo wameiomba serikali itatue tatizo hilo ili wananchi wapate huduma bora za kijamii.

Wakitoa malalamiko yao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wamesema kuwa licha ya uuzaji holela wa ardhi kuna migogoro ya ardhi katika kata hiyo na wananchi wengi wanaomiliki ardhi bado hawajapatiwa hati jambo ambalo linawapa wasiwasi kuwa huenda ardhi zao zikamegwa na wawekezaji

Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Joseph Kamete alisema kuwa wameomba sana hati za maeneo ambayo wanaishi lakini wamekuwa hawapewi na wanazungushwa zungushwa kitu ambacho kinawatia mashaka makubwa.

“Mkuu wa Mkoa kinachotuuma zaidi sisi tumekaa hapa tangu kipindi cha mikonge lakini tukiomba hati hatupewi lakini akija muwekezaji anapatiwa hati kwa wakati sasa tunajiuliza inamaana sisi atuna haki ya kukaa katika viwanja hivi watuambie tu ili na sisi tujue sio wanafanya kazi ya kutuzungusha zungusha kwakweli tumekuwa tunaishi kama ndege katika maeneo yetu na atuna amani kabisa maana kama wanatunyima hati wanania gani kweli tunaomba mkuu wa mkoa utusaidie kwa hili “alisema Zaituni Marunda.

Aidha wananchi hao pia wanasumbuliwa na kero za maji na umeme kwa kipindi kirefu hivyo wameiomba serikali iwasaidie kutatua kero hiyo inayowaathiri zaidi kinamama ambao hutembea umbali mrefu wakitafuta huduma za maji.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiwa na Muwekezaji Hans Paul (kulia), pamoja na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Athuman Kiamia wakipiga magofi mara baada ya kuzindua daraja.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ambaye alifika katika kata hiyo katika shughuli ya uzinduzi wa daraja lililojengwa na mwekezaji Hans Paul ameagiza ofisi ya Mkurugenzi kumkabidhi ripoti ya maeneo ya wazi ya jiji yaliyouzwa kienyeji ili aweze kushughulikia kero hiyo pia ameshukuru kampuni ya Hanspaul kwa kujitoa kusaidia jamii jambo ambao linapaswa kuigwa na wawekezaji wengine.


Alisema kuwa wao kama serikali wapo tayari kushirikiana na wawekezaji ambao wanalipa kodi kama ipasavyo na wale ambao wanajishuhulisha katika kusaidia jamii inayowazunguka.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha amefanya mkutano wa kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi pamoja na kuzindua daraja ambalo limegharimu kiasi cha shilingi milioni 67.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo akiongea na wananchi wa kata ya Engutoto iliyopo ndani ya jiji la Arusha.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad