Mtaa Kwa Mtaa Blog

TANZANIA YAPIGA HATUA KUBWA KATIKA HUDUMA ZA UZAZI WA MPANGO

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Juu ya kuboresha huduma za uzazi wa mpango nchini tofauti na kipindi cha nyuma ili kuondoa idadi ya ongezeko kubwa la watu na kupunguza vifo kwa wajawazito na watoto kama sera ya Afya ya mwaka 2007 inavyosema. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mpoki Ulisubisya.
Rais wa Mpango wa Maendeleo kutoka Taasisi ya Bill & Melinda Gates Foundation ya Maerekani, Christopher J. Elias akizungumza machache wakati wa akifungua mkutano wa Bodi kwa nchi zilizoamua kuongeza idadi ya watu wanaofahamu uzazi wa mpango kundi linalojulikana kama "FP 2020 Reference Group,jiji Dar es Salaam.
Baadhi ya viongozi mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya ufunguzi wa mkutano wa Bodi kwa nchi zilizoamua kuongeza idadi ya watu wanaofahamu uzazi wa mpango kundi linalojulikana kama "FP 2020 Reference Group. jiji Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii


Na Ally Daud-MAELEZO           
Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuboresha huduma za uzazi wa mpango nchini tofauti na kipindi cha nyuma ili kuweza kuondoa idadi ya ongezeko kubwa la watu na kupunguza vifo kwa wajawazito na watoto kama sera ya Afya ya mwaka 2007 inavyosema.            

Hayo yamesemwa na Waziri Ummy Mwalimu(Mb) hivi karibuni wakati akifungua mkutano wa Bodi kwa nchi zilizoamua kuongeza idadi ya watu wanaofahamu uzazi wa mpango kundi linalojulikana kama "FP 2020 Reference Group.

“Tanzania imepiga hatua kubwa katika kuboresha huduma za uzazi wa mpango nchini tofauti na kipindi cha nyuma ili kuweza kuondoa idadi ya ongezeko kubwa la watu na kupunguza vifo kwa wajawazito na watoto kama sera ya Afya yam waka 2007 inavyosema” alisema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa mkutano huu unafanyika kwa mara ya kwanza barani Afrika na hususani katika ardhi ya Tanzania hii ni kutokana na mafanikio makubwa yaliyofikiwa katika eneo hili la uzazi wa mpango.

Waziri Ummy amesema kuwa mafanikio hayo ni pamoja na ongezeko la bajeti katika eneo la uzazi wa mpango na kupunguza hali utegemezi kwa kiasi kikubwa kutoka kwa wahusani,kuimarisha mìfumo ya usambazaji wa dawa na vifaa tiba za uzazi wa mpango hapa nchini.

Mbali na hayo Waziri Ummy alieleza kuwa katika mikoa ya kanda ya ziwa  na magharibi mwa nchi kumekuwa na ongezeko la uelewa na utumiaji wa huduma za uzazi wa mpango kama vile mkoa wa Mara kuna ongezeko la utumiaji kutoka asilimia 10 hadi asilimia 29 kuanzia mwaka 2010 hadi 2015 na katika mkoa wa kagera kumekuwa na ongezeko kutoka asilimia 24 hadi asilimia 39.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya uzazi wa mpango Dkt.Babatunde  alipongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya  nchi yetu katika kuhakikisha huduma hii inaimarika.

Mkutano huo wa siku tano ulioanza Oktoba 31 hadi  Novemba 4 mwaka huu unahudhuriwa na wajumbe na wadau kutoka nchi mbalimbali duniani ikiwa na lengo la kujadili fursa mbalimbali na changamoto zilizopo katika eneo la afya ya uzazi wa mpango duniani.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget