HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, November 11, 2016

MKE WA RAIS MAMA JANETH MAGUFULI ARUHUSIWA KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIPOKUWA AMELAZWA

 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwa anatoka kwenye  Wodi ya Sewahaji katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kurejea nyumbani  mara baada ya kuruhusiwa baada ya kupata nafuu. Mama Janeth Magufuli alikuwa amelazwa hospitalini hapo tangu tarehe 9 Novemba 2016.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Raymond Mwenesano, Mkuu wa Idara ya Wagonjwa wa nje na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Edward Ngwalle, Daktari wa Rais mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitalini hapo na kurejea nyumbani baada ya kupata nafuu.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akimshukuru Dkt. Benard Kepha ambaye Daktari Bingwa wa Magonjwa ya dharura na ajali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili mara baada ya kuruhusiwa kutoka na kurejea nyumbani mara baada ya kupata nafuu. Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad