Mtaa Kwa Mtaa Blog

KONGAMANO LA PANDA LAWAKUTANISHA WANAFUNZI WA KIKE TOKA VYUO MBALIMBALI NCHINI

Mwanzilishi wa Taasisi ya Her Initiative, Lydia Charles (kushoto) akimtambulisha Mwenyekiti mpya wa Taasisi hiyo, Irene Enock wakati wa Kongamano la siku moja lililowajumuisha wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali na vyombo vya habari, likiwa na lengo la kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo. Kondamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Yombo 4 ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Her Initiative iliyojulikana mwanzo kama Teen Girls Supportive Initiative (TGSI) kwa kushirikiana na DUMA waliandaa Kongamano lililojulikana kama Panda. Kongamano hilo liliwajumuisha wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali na vyombo vya habari yote katika lengo la kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo.

Her Initiative ni asasi ya wasichana ambayo ndio mhimili wa maongezi. Her Initiative inawapa wasichana nafasi ya kuwakilisha na kusimamia maswala yao wenyewe ya kiuchumi, elimu, kiutamaduni na kiafya, na inamjengea uwezo msichana wa kutafuta suluhu ya changamoto zake mwenyewe bila kutegemea watu wengine. Vyote hivi hufanyika kupitia kampeni, matamasha, semina na kuwapa msaada wa mahitaji ya kielimu, kiuchumi na kiafya kwa kushirikiana na wadhamini mbalimbali.

Panda ni event inayohusu ujasiriamali, uvumbuzi, ubunifu na matumizi mazuri ya pesa. Kama tunavyofahamu, wasichana tuna matumizi mengi ya pesa na mara nyingi matumizi haya huzidi kipato cha pesa tunachokipata. Kwa kuona hilo wasichana hao waliamua kuandaa tamasha ili kusaidiana kuepuka hatari zinazoweza kutokana na kutokuwa na uchumi imara. Madhumuni ni kumjengea msichana hali ya kujitegemea kwa kumfundisha namna ya kuhifadhi pesa kupitia benki tofauti na mifuko mbalimbali ya jamii.

Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Yombo 4 ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, ulifunguliwa na Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini, Mboni Mhita ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hii. Wageni wengine waliohudhuria na kutoa maneno ya ushauri kwa wasichana ni pamoja na Dr. Sebastian Ndege "CEO wa Jembe Group ", Shekha Nasser wa Shear Illusions, Irene Kiwia mwanzilishi wa Frontline Portel Novelli, Vanessa Mdee Mwanamuziki,Mc Pilipili Mchekeshaji, Idriss Sultan Mchekeshaji na Millard Ayo mmiliki wa online Television.
Mbunge wa Jimbo la Handeni Vijijini, Mboni Mhita ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika Kongamano hilo, akitoa nasaha zake kwa wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini katika kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jembe Group, Dkt. Sebastian Ndege akitoa mada katika Kongamano la siku moja lililowajumuisha wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali na vyombo vya habari, likiwa na lengo la kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo. Kondamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Yombo 4 ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Shear Illusions, Shekha Nasser akitoa mada katika Kongamano la siku moja lililowajumuisha wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali na vyombo vya habari, likiwa na lengo la kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo. Kondamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Yombo 4 ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Mwanzilishi wa Kampuni ya Frontline Portel Novelli, Irene Kiwia akitoa mada katika Kongamano la siku moja lililowajumuisha wanafunzi wakike kutoka vyuo mbalimbali nchini pamoja na wadau mbalimbali wanaojishughulisha na biashara, ujasiriamali na vyombo vya habari, likiwa na lengo la kukuza upeo na uelewa wa wasichana katika maswala mbalimbali ya maendeleo. Kondamano hilo lilifanyika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa Yombo 4 ndani ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

Timu ya wasichana kutoka Her initiative.
Baadhi ya wasichana waliohudhuria wakifatilia mada mbalimbali zililokuwa zikitolewa ukumbini hapo. 
Meza kuu.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget