HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, November 6, 2016

HUDUMA YA UPANDIKIZWAJI WA VIFAA VYA USIKIVU YAANZA RASMI NCHINI.

Na Ally Daud-MAELEZO
HUDUMA ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto imeanza kutolewa rasmi nchini  katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili  baada ya wataalamu wa huduma hiyo kurejea wakitokea mafunzoni nchini India ili kuweza kusaidia watanznia hususani watoto wenye matatizo ya kusikia .
Akizindua huduma hiyo kwenye hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Uisubisya amesema kuwa  Huduma hiyo imekua hadimu nchini hivyo kufanya kugharamia kiasi kikubwa cha fedha kwenda kuwatibia nje ya nchi.
“Kwakweli huduma hii ya kupandikiza watoto vifaa vya usikivu italeta msaada mkubwa kwa watanzania na kuokoa gharama takribani shilingi milioni 80 kwa kila mtoto ambaye alitakiwa kwenda kutibiwa nje ya nchi” alisema Dkt. Ulisubisya.
Aidha Dkt. Ullisubsya amesema kuwa wazazi wanatakiwa kuwa mstari wa mbele kugundua mapema matatizo ya watoto na kuwaleta katika Hospitali ya Muhimbili ili wapate taratibu za kupata huduma hiyo bila ya kuchelewa na kpata madhara makubwa.
Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru amesema kuwa Huduma hiyo ambayo ilikua inafuatwa nje ya nchi sasa inafanyika nchini ikiwa ni jitihada za serikali katika kuokoa gharma za matibabu ya nje ya nchi.
Aidha Prof. Museru amesema kuwa hadi kufikia Januari 2017 MNH itaanza kufanya upasuaji na kupandikiza vifaa vya usikivu ikiwa ni huduma iliyokamilika bila ya kwenda nje ya nchi hivyo kupelekea kupunguza gharama zaidi na kusogeza huduma karibu.
“Hapa tulipofikia sio mwisho wa kutoa hudum hii , tunataka kufikia Januari 2017 tuwe tunafanya upasuaji kabla ya kupandikiza vifaa vya usikivu ikiwa ni huduma kamili na tutakuwa tumefikia baadhi ya malengo tuliyojiweka mpaka kufikia muda huo” alisema Prof. Museru
Aidha Prof. Museru amesema kuwa Serikali ilianza jitihada  za kuileta huduma hii nchini miaka mitatu iliyopita kwa kushirikiana na kampuni ya kuuza vifaa vya kupandikiza vifaa vya usikivu ya Medel kutoka nchini Misri.
Kwa upande wa Mzazi wa mtoto aliyepandikizwa kifaa cha usikivu Angel Ibrahimu (4) mkazi wa Mbeya amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa jitihada zake za kufanikisha huduma hiyo kwa mtoto wake kwani lilikua tatizo ambalo hakuweeza kulitatua kwa uwezo wake.
Katika ufunguzi wa huduma hiyo ambayo itakua endelevu nchini imepandikiza vifaa vya usikivu kwa watoto 16 ambao wapepunguza gharama ya kwenda nje ya nchi takribani shilingi milioni 300 ambazo zitaenda kwenye huduma nyingine za maendeleo ya jamii. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika leo jijini  Dar es salaam, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru.
 Mkurugenzi wa kampuni inayotoa huduma na kuuza vifaa vya usikivu ya Medel Bw. Mohamed Disouky wa kwanza kushoto akimpa maelezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya wa pili kulia jinsi huduma hiyo inavyotolewa wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika leo jijini Dar es salaam, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence 
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Muhimbili Prof. Lawrence Museru akiongea na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika jijini Dar es salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya.
 Baadhi ya wazazi wa watoto wenye matatizo ya usikivu wakiwa katika foleni ya kusubiri huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu wakati wa uzinduzi wa huduma ya upandikizwaji wa vifaa vya usikivu kwa watoto uliofanyika jijini Dar es salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jami

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad