Mtaa Kwa Mtaa Blog

FAINALI ZA “VALEUR COMEDY NIGHTS” MUSIMU WA PILI KUFANYIKA NOVEMBA 19 2016

Kampuni ya Tanzania Distilleries Limited (TDL) kupitia chapa yake ya ‘Valeur Superior Brandy’, kwa kushirikiana na kampuni ya Vuvuzela Company Ltd, wanatangaza rasmi fainali ya shindano la “Valeur Comedy Nights” msimu wa pili, ambalo ni shindano la kusaka vipaji vya sanaa ya uchekeshaji.

Fainali hiyo inatarajiwa kufanyika Jumamosi tarehe 19 Novemba 2016, Katika ukumbi wa 40/40 Baa, Tabata ambapo kutakuwa na washiriki 18 waliopatikana kutoka katika fainali za wilaya za mkoa wa Dar es Salaam. Mashindano haya ni kusaka mshindi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumuza na waandishi wa Habari, Meneja wa Kanda wa Mauzo na Usambazaji wa Kampuni hiyo, Mwesige Mchuruza alisema, “Msimu wa pili wa “Valeur Comedy Nights” umeendelea kupokelewa vizuri na wateja wetu. Kutokana na kwamba huu ni msimu wa pili, wateja wanalifahamu vizuri shindano hili na tumeona wacheheshaji wengi wakijitokeza kushindana. Washirika wetu kutoka Kampuni ta Vuvuzela Company Ltd kwa mara nyingine tena wametoa msaada mkubwa kwani wamewapa washiriki mafunzo na kuwatayarisha kwa fainali hizi”.

Mashindano hayo yalianza Septemba 6, 2016 yakijumuisha zoezi la kusajili watu kushiriki katika mashindano hayo.

Mchuruza aliendelea kusema mshindi wa ‘Valeur Comedy Nights’ atapata pesa taslimu 2,000,000/= na mafunzo ya vitendo ya miezi 6 na Evans Bukuku katika kampuni yake ya Vuvuzela Company Ltd.
Meneja Mauzo na Usambazaji Kinywaji cha Valeur kutoka Kampuni ya TDL, Mwesigwa Mchuruza akimkabidhi Hundi ya Shilingi Milioni Mbili Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vuvuzela, Evans Bukuku ikiwa zawadi ya mshindi wa kwanza kwa mshindi atakayepatikana katika fainali shindano la kuchekesha linayolotarajiwa kufanyika jumamosi Oktoba 19,2016 Katika Bar ya 40/40 iliyoko Tabata jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vuvuzela, Evans Bukuku(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa kutangaza zawadi za washindi katika fainali zinazotarajiwa kufanyika jumamosi Oktoba 19,2016 Katika Bar ya 40/40 iliyoko Tabata jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja Mauzo na Usambazaji Kinywaji cha Valeur kutoka Kampuni ya TDL, Mwesigwa Mchuruza.Kulia ni mshindi wa Mwaka jana, Hussein Athuman.
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget