Mtaa Kwa Mtaa Blog

YANGA YAICHAPA JKT RUVU BAO 4-0 BILA KOCHA WAKE MKUU

TIMU ya soka ya Yanga imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 4-0 dhidi ya JKT Ruvu na kufikisha jumla ya alama 24 na kuendelea kusalia katika nafasi ya pili ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Yanga walioanza kuona goli la JKT Ruvu dakika ya sita ya mchezo kupitia kwa Obrey Chirwa lakini umakini mbovu wa safu ya washambualiaji ulifanya wakose magoli mengi na mpaka kumalizika kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza Yanga walitoka mbele kwa goli 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kulisakama lango la JKT Ruvu na katika dakika ya 63 Amisi Tambwe aliyeingia kuchukua nafasi ya Donald Ngoma aliiandikia Yanga goli la pili na dakika ya 83 Simon Msuva kwa kutumia udhaifu wa golikipa Said Kipao aliyekuwa mwiba kwa safu ya ushambuliaji wa Yanga akaweka kimiani goli la tatu.

Safu ya ushambuliaji ya JKT Ruvu wanashindwa kuwa makini ambapo wanashindwa kufanya mashambulizi ya uhakika na mabeki wa Yanga kuweza kusahihisha makosa yao.

Dakika ya 90, Amisi Tambwe anaiandikia Yanga goli la nne na kupeleka kilio zaidi kwa JKT Ruvu na mpaka dakika 90 zinamalizika Yanga wanatoka mbele kwa goli 4-0.

Yanga imecheza leo chini ya Kocha Juma Mwambusi baada ya Aliyekuwa kocha mkuu Hans Van De Pluijm kujiuzulu jana jioni.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amis Tambwe akishangilia mara baada ya kupatia timu yake bao la pili, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu, uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo na kuifanya timu ya Yanga kuondoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 4-0.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Amisi Tambwe akiachia mkwaju mkali uliotinga moja kwa moja wavuni na kupatia timu yake bao la pili, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Ruvu, uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam leo na kuifanya timu ya Yanga kuondoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 4-0.
Simon Msuva wa Yanga akiachia shuti lililoelekea moja kwa moja wavuni na kuiandikia timu yake bao la tatu dhidi ya Timu ya JKT Ruvu, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara, uliopigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.
Wachezaji wa Yanga wakishangilia ushindi wao kwa mtindo wa ku 'dub'.

Hassan Kessy wa Yanga akiichambua ngome ya Timu ya JKT Ruvu, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliopigwa leo katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam.


Kocha wa Yanga alieyejiuzulu, Hans Van Plujin akiwa jukwaani kuwaangalia vijana wake.
Kocha wa Yanga, Juma Mwambusi akiwa na Meneja wa Timu hiyo pamoja na Kocha wa Makipa.


Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget