HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 17, 2016

Wananchi waiomba NHIF kundeleza huduma za upimaji afya

Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Shinyanga na Simiyu Bw. Imanuel Amani akitoa elimu kwa mwananchi mkoani Simiyu aliyefika katika banda la Mfuko kujua namna ya kujiunga. 

Na Mwandishi Wetu, Simiyu

WANANCHI wa Mkoa wa Simiyu wameuomba Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuendelea kutoa huduma ya upimaji wa afya bure katika maeneo ya vijijini ili wananchi walioko huko wanufaike nazo.

Rai hiyo waliitoa mwishoni mwa wiki iliyopita katika kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Vijana iliyofanyika mkoani humo ambapo Mfuko ulitoa huduma za upimaji wa afya zikiambatana na uhamasishaji wa wananchi kujiunga na huduma zake.

“Kama unavyoona wananchi walivyojaa hapa kupata huduma za upimaji...hii ni ishara kwamba huduma hizi zinatakiwa zaidi hasa huko vijijini ambako fursa kama hizi imekuwa ni ngumu kuzipata hivyo Mfuko uangalie namna ya kuendelea kutuletea hii huduma,” alisema Mkazi wa Bariadi Bw. Masunga Maduhu.
Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma, Grace Michael akitoa huduma ya uelimishaji wa wananchi waliotembelea banda la Mfuko. 

Hata hivyo walipongeza kitendo kilichofanywa na Mfuko cha kutoa huduma katika maadhimisho hayo ambayo imesaidia wananchi wengi zaidi kutambua hali ya afya zao lakini pia wamenufaika na elimu kutoka kwa wataalam ya namna ya kuepukana na maradhi yasiyoambukiza.

Mfuko ulitoa huduma za vipimo vya shinikizo la damu, kiwango cha sukari, uzito na urefu ambapo jumla ya wananchi 1,311 walipata huduma ya upimaji wa afya. Kati ya wananchi hao 175 walionekana kuwa na matatizo ya uzito, wananchi 30 matatizo ya sukari na wananchi 43 matatizo ya shinikizo la damu.

Kwa upande wake Meneja wa NHIF Mkoa wa Shinyanga na Simiyu Bw. Imanuel Amani alisema kuwa huduma za upimaji hufanywa mara kwa mara katika maeneo mbalimbali hivyo akawaomba wananchi wanapokutana na fursa kama hizo wazitumie.

“NHIF tuna mpango wa elimu ya Kata kwa Kata ambayo mbali na uhamasishaji huwa tunatoa huduma za upimaji wa afya hivyo Mfuko umetoa kipaumbele kikubwa katika suala hili,” alisema.
Wananchi mbalimbali wakiendelea kuhudumiwa katika banda la Mfuko lililotoa huduma za upimaji wa afya bure katika maadhimisho ya wiki ya Vijana mkoani Simiyu.
Huduma za upimaji zikiendelea.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Shinyanga na Simiyu Bw. Imanuel Amani akizungumza na wananchi waliofika kupata huduma za upimaji.
Wananchi walifurika katika banda la Mfuko kwa lengo la kupata huduma.
Wananchi wakijiandikisha kupata huduma.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad