HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 31, 2016

Wananchi Bupigu waiomba Serikali kuongeza nguvu katika kilimo cha umwagiliaji

Na Humphrey Shao, Ileje

Wakazi wa Kata ya Bupigu Wilayani Ileje wameiomba Serikali kuongeza nguvu katika kilimo cha umwagiliaji kwa wakazi wa eneo hilo hili kupunguza tatizo la njaa wilayani humo.

Hayo yamesemwa na Katibu wa kikundi Nguvu kazi, Isaka Kamwela, kinachojihusisha na kilimo cha umwagiliaji katika kata hiyo kwenye  Mto Mtumbisi.

“tumekuwa tukilima kwa kumwagilia kwa kipindi cha misimu minne kwa mwaka hali inayowafanya wakulima kuwa na fedha za kujikimu lakini uzalishaji umekuwa mdogo kutoka na kukosa elimu ya kutosha juu ya kilimo hicho” amesema Kamwela.

Amasema kuwa wamekuwa wakikutana na changamoto nyingi sana hasa za masoko pindi wanapolima bidhaa za mbogamboga na kuishia kuoza mashambani bila kupata wateja.

Amaeongeza kuwa ni vyema serikali ikawatuma wataalam wa masuala ya usindikaji mazao kwenda kutoa elimu ya kutosha kupunguza hasara wanayopata wa kulima.
sehemu ya wanachama wa kikundi cha umwagiliaji cha nguvu kazi wakiendelea na kilimo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad