Mtaa Kwa Mtaa Blog

WADAU WA MASUMBWI WAMFARIJI BABA WA BONDIO THOMAS MASHALI LEO

 Mzazi wa marehemu Thomas Mashali, Malifeza Mashali (wa pili kulia) akizungumza na aliyekuwa Promota wa mtoto wake, Kaike Siraju (kulia) wakati Promota huyo alipofika kwenye msiba leo nyumbani kwa mzee huyo maeneo ya Tandale jijini Dar es Salaam. Marehemu Mashali enzi za uhai wake alishasainiana mkataba na Promota huyo wa kupanda ulingoni mwezi wa 12 kwa pambano la Ubingwa wa Dunia dhidi yake na Bondia kutoka Malawi, Chimwemwe Chiota. 
Katika pambano hilo ambalo lingekuwa la utangulizi lingebebwa na pambano kubwa ambapo litawakutanisha mabondia Francis Cheka na Dullah Mbabe litakalopigwa mjini Morogoro. 

Kwa mujibu wa Baba Mzazi, Malifeza Mashali aliesema kuwa Marehemu anatarajiwa kuzikwa keshokutwa katika makaburi ya Kinondoni baada ya taratibu na sheria za Kipolisi kumalizika kutokana na mazingira ya kifo cha bondia huyo. Kushoto ni mdogo wa marehemu.
 Sehemu ya majirani ndugu na marafiki wakiwa katika msiba huo.
  Sehemu ya majirani ndugu na marafiki wakiwa katika msiba huo.
 Baba wa marehemu akipokea simu nyingi kuhusu msiba huo leo

  Sehemu ya majirani ndugu na marafiki wakiwa katika msiba huo.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget