HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 3, 2016

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA CUBA, IKULU JIJINI DAR LEO

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa (kulia kwake) na ujumbe wake alipokutana nae Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2016. Makamu wa Rais wa Cuba, yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu yenye lengo la kuendeleza na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, utamaduni, michezo, kilimo, nishati, teknolojia na kuangalia maeneo mapya ya uwekezaji.
Makamu wa Rais, Mh. Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia walioketi) akiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Cuba, Salvador Antonio Valdes Mesa (wa tatu kushoto walioketi) wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wao, mara baada ya mazungumzo, Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 3, 2016. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad