Mtaa Kwa Mtaa Blog

MABADILIKO YA SHERIA NI CHACHU YA KUPUNGUZA AJALI ZA BARABARANI

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

SHERIA ya usalama Barabarani ya mwaka 1973 imekuwa na haina sheria madhubuti ya kukabiliana na ajali za barabarani huku waandishi wa habari wakitakiwa kuandika makala zenye kujenga hoja na umuhimu wa usalama barabarani.

Kwa mujibu wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani kupitia kwa mjumbe wake Henry Bantu amesema kuwa ajali za barabarani zinasababishwa na hazitokei kama watu  wanavyosema na hilo linatokana na madereva wengi hawajatayarishwa kutumia barabara.

Bantu amesema, kila barabara ina vipimo vyake na kuna barabara ni ya mwendo kasi na mwendo wa kawaida na mfumo wa barabara nchi si salama kwani kuna makundi ambayo yanatakiwa kushirikiana kwa ufanisi mkubwa sana ili kuweza kupunguza ajali za barabarani.

Wahandisi ambao lengo lao kubwa ni kujenga barabara yenye viwango vinavyopendekezwa na vyenye hali ya juu wanatakiwa washirikiane vizuri na watoa elimu kwa ajili ya kuwaelimisha matumizi sahihi kabisa ya matumizi sahihi ya barabara huku vyombo vya usalama wakihusika katika kuwakamata wanaovunja sheria.

Waandishi wa habari, wanasiasa, mashirika ya bima wanatakiwa kutoa hamasa katika utoaji wa elimu kwa jamii inayomzunguka kutokana na kuwa na chachu katika kuelimisha wananchi wake, pia dharula ikiwemo gari ya wagonjwa, huduma ya kwanza zitasaidia katika kupunguza vifo vya majeruhi pale inapotokea ajali kwani kumekuwa na kutokuwa na utayari au kujiandaa na ajali zinazotokea.

Ili kuepukana na ongezeko la ajali hizi, Baraza la Taifa la Usalama halina budi kufanya marekebisho ya  Sheria ya mwaka 1973 ili kuweka sheria kali zitakazowabana madereva na watumiaji wa barabara.
Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani Henry Bantu akitoa maelezo ya sheria za barabarani wakati wa semina elekezi kwa waandishi wa habari iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa habari Wanawake (TAMWA)

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget