Mtaa Kwa Mtaa Blog

MAANDALIZI ROTARY DAR MARATHON 2016 YAKAMILIKA


Mbio na matembezi ya hisani za Dar rotary marathon zinatarajiwa kufanyika siku ya ijumaa tarehe 14.10.2016 katika viwanja vya Green, Oysterbay hapa jijini Dar es salaam kuanzia saa 12 asubuhi ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa rais mstaafu mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi. 

Mbio na matembezi hayo yameandaliwa na klabu sita za Rotary za hapa Dar es salaam kwa kushirikiana na Benki M na kauli mbiu ya mwaka huu ni “kuponya maisha, badilisha jamii” ambapo fedha zitakazochangishwa ziltaelekezwa katika ujenzi wa hospitali ya mafunzo hapa Dar es salaam.
Kutakuwa na matembezi ya kilomita 5 kwa ajili ya familia, kilomita 9 na mbio za kilomita 21.1 nusu marathon, halikadhalika kutakuwa na waendesha baiskeli.

Kushiriki unaweza kujisali kupitia vituo vifuatavyo: Shoppers Plaza supermarkets in Masaki, Mikocheni and Mbezi; Slipway; Mlimani City; Shrijee Supermarket Masaki, City Mall; Oysterbay Shopping Centre; Collosuem masaki; JM Mall and Kibo Complex Tegeta.     
Washiriki mbalilmbali walijitokeza kushiriki matembezi ya Rotary Dar Marathon mwaka jana, hali iliyopelekea matembezi hayo kufana sana.
Labels:

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget