Mtaa Kwa Mtaa Blog

HALOTEL YASHEREHEKEA KUADHIMISHA MWAKA MMOJA WA HUDUMA YA MAWASILIANI NCHINI, YAZINDUA HUDUMA MPYA YA HALOPESA

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Halotel Tanzania, Le Van Dai (katikati), Afisa Mtendaji wa Halotel Tanzania, Henry Mavulla (mwenye tai), Afisa Mawasiliano wa Halotel Tanzania, Stella Pius wakikata keki kwa pamoja ikiwa ni ishara ya kusherehekea kuadhimisha mwaka mmoja wa kutoka huduma ya mawasiliano hapa nchini na kuzindua huduma yao mpya ya ya HALOPESA, hafla hiyo imefanyika leo Oktoba 13, 2016 kwenye ofisi zao zilizopo eneo la Kinondoni Moroco, jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni sehemu ya wafanyakazi wa Kampuni hiyo walioshiriki kwenye hafla hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Halotel Tanzania, Le Van Dai akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla yao ya kusherehekea kuadhimisha mwaka mmoja wa kutoka huduma ya mawasiliano hapa nchini na kuzindua huduma yao mpya ya ya HALOPESA, ambapo alisema kuwa lengo la Kampuni hiyo ni kuhakikisha wanawazidi washindani wao katika soko na ndio maana huduma zao zimekuwa zikipokelewa vyema sokoni.
Afisa Mawasiliano wa Halotel Tanzania, Stella Pius akizungumza na waandishi wa habari, juu ya kampuni yao inavyoendelea kuboresha miundombinu ya kijamii kama vile utoaji wa huduma ya bure ya mtandao wa intaneti kwa shule 450 hapa nchini (zenye umeme) kwa kipindi cha miaka mitatu.

Post a Comment

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget